Ilunga Makabu kulia, akiwa na mpinzani wake, Gogito Gorgiladze.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAPAMBANO mawili yenye mguso wa aina yake Bara
la Afrika, yamefanyika katika majiji mawili ya Johennsburg, Afrika ya Kusini na
Tunis, Tunisia, kwa kushirikisha miamba miwili, kati ya Ilunga Makabu, mwenye
asili ya nchini Kongo na Gogito Gorgiladze wa Georgia, mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Ilunga Makabu
Katika pambano hilo la raundi nne, lilikuwa la
kugombea Ubingwa wa Dunia wa vijana walio chini ya miaka 25 katika uzito wa
Cruiserweight, ambapo Makabu aliibuka na ushindi katika patashika hiyo.
Taarifa iliyotumwa
katika vyombo vya habari na Rais wa Shirikisho la Ngumi Afrika na Ghuba ya
Uajemi, ambaye pia alikuwa mmoja wa waamuzi katika pambano hilo, Onesmo Ngowi,
ilisema kuwa mambo yalianza kujionyesha katika raundi ya kwanza tu wakati
bondia Makabu alipokuwa anarusha ngumi ya mkono wa kushoto ambayo ilikuwa
inafanya madhara yasiyojificha kwa Gogito.
Katika raundi ya pili na
ya tatu Gogito alikuwa anarudi nyuma na kuongea kana kwamba anamwambia Illunga asimwadhiri
mbele ya watu lakini Mkongo man Makabu alisonga mbele akirusha makonde mazito
bila huruma.
Ilipoanza raundi ya nne
(4) Ilunga alirusha makonde sita ya kasi ambayo yalimfanya referee wa mpambano
huo Wally Snowball wa Afrika ya Kusini kuingialia kati na kusimamisha mpambano
huo!
Golden Gloves ya Rodney
Berman ndiyo iliyoandaa mpambano huo na Illunga amepangwa kuteta taji lake
mwezi ujao nchini Monaco katika tamasha la “The Last Man Standing”
litakalofanyika katika jiji la Monte Carlo.
Katika pambano la nchini
Tunisia, bondia kutoka nchini Belgium, Ayoub Nefzi, alimtwanga mpinzani wake
mwenye asili ya nchini Ghana, Ishmael Tetteh, katika raundi ya 7, ambapo
walipigana katika jiji la Tunis na kuvutia hisia za wengi.
Mpambano huo ulikuwa wa
kugombea Ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya
kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Jr. Middle na uliandaliwa na Halmashauri ya
jiji la Tunis katika juhudi zake za kukuza ‘Utalii wa Michezo’.
No comments:
Post a Comment