https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, February 14, 2013

Misa ya maziko ya kumuombea Askofu Amedeus kuhudhuriwa na Rais Kikwete

Misa Takatifu ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi Amedeus Msarikie inaendelea katika Kanisa la Kristo Mfalme Moshi mkoani Kilimanjaro. 
Misa ya Leo inaongozwa na Baba Askofu Tarsisius Ngalalekumtwa ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Tanzania. 

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Kanisa hilo imesema majira ya saa 7: 30 mchana huu kutafanyika Maziko katika Kanisa la Kristo Mfalme Moshi ambapo Mwili wa Marehemu Amadeus Msarikie utazikwa.

Ibada hiyo ya maziko itahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kanisa, viongozi wa Kisiasa nchini, Viongozi wakuu wa Serikali wakiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
 
Viongozi mbalimbali ulimwenguni wametoa salamu zao za rambirambi kufuatia msiba huo mkubwa wa Kanisa Katoliki akiwemo Balozi wa Papa nchini Tanzania.

Itakumbukwa kwamba mwishoni mwa mwaka 2012 Marehemu Askofu Amedeus Msarikie aligundulika kuwa na ugonjwa wa saratani na mwanzoni mwaka huu alipelekwa Mjini Nairobi kwa ajili ya matibabu ambapo alifariki Februari 7 akiwa na umri wa miaka 82.

Baba Askofu Ngalalekumtwa ametaja Marehemu Msarikie kama kiongozi wa kuigwa ambaye aliwekeza katika elimu pia miaka 52 aliitumia katika Upadre na miaka 27 katika nafasi ya Uaskofu ndani ya kanisa hilo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...