Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BINGWA wa IBF katika bara la Afrika uzito wa unyoya
(Featherweight) Ramadhani Shauri, amepewa nafasi ya kugombea ubingwa wa Dunia wa
IBF kwa vijana walio chini ya miaka 25 uzito wa Lightweight.
Shauri ambaye
alishinda taji la ubingwa wa IBF katika bara la Afrika mwaka jana baada ya
kumpiga bondia Sunday Kizito wa Uganda ana rekodi ya mapambano 17.
IBF imeamua kumpatia Shauri nafasi ya kugombea ubingwa huo
wa dunia kwa vijana baada ya kuangalia mkanda wa video wa pambano lake la
ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,
Mabondia wengi wa Marekani ambao walikuja kuwa mabingwa wa
dunia na kuweza kupata pesa nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana
na hivyo kuweza kupanda chati kwenye viwango vya IBF. Mbondia hao ni kama
Bernard Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la Hoya.
Kama Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa
vijana atakuwa kwenye macho ya mapromota wakubwa duniani kama kina Dong King,
Bob Arum na wengine wengi.
Nafasi kama hii inaipa nchi ya Tanzania nafasi nzuri sana ya
kujitangaza kibiashara na utalii kwani dunia inaiona kuwa kati ya nchi
zinazotoa mabingwa wa dunia.
Kama Shauri atashinda taji hili atakuwa Mtanzania wa kwanza
tangu historia ya ngumi nchini kuweza kushinda taji la shirikisho kubwa kati ya
manne duniana ambayo ni IBF, WBA, WBO na WBA.
Shiriksiho la Ngumi la Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo
lina makao yake makuu ya kuhudumia bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki
ya Kati ndilo lililomtafutia Shauri nafasi aliyopata.
IBF/Africa inawahamasisha Watanzania walio na mapenzi mema
na nchi yao pamoja na makampuni mbalimbali bifsi ya umma yajitokeze kwa wingi
kumpatia Shauri ufadhili wa kuweza kuligombea taji hili.
No comments:
Post a Comment