Diamond akiwa na demu wake mpya.. Uhusiano wao huu umeanza kwa mbwembwe nyingi, ingawa jamaa anazuga kama kawaida yake.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, Diamond,
ameshangaza watu kwa kitendo chake cha kuendekeza kuvua nguo watoto wa watu,
ikiwa ni tabia inayozidi kuota mizizi kwa mkali huyo.
Diamond na Jokate Mwigelo enzi za uhusiano wao
Hadi sasa, Diamond ametoka kimapenzi na wasichana kibao,
akiwamo Wema Sepetu, Jokate Mwigelo na sasa yupo na Vj Penny, uhusiano ulioanza
kwa mbwembwe lukuki.
Wema Sepetu, akiongea kwa jazba.
Jana usiku alipokuwa akizungumza katika kipindi cha mapenzi
kinachorushwa na Clouds FM, kinachoongozwa na mtangazaji wake, Diva, Diamond
alionekana kujikanyaga zaidi kwa kushindwa kuzuia hisia zake kwa akina dada.
Diva alimuuliza Diamond idadi aliyowavua nguo mabinti, swali
ambalo lilionyesha kuwakera watu wengi waliokuwa wakifuatilia. Kwa kipindi cha
miaka miwili sasa, stori zote za msanii huyo zimekuwa zikihusiana na wanawake
kama ilivyokuwa kwenye nyimbo zake nyingi kuwa za mapeni.
Hata hivyo, anapobanwa, mkali huyo hudanganya kuwa ni rafiki
tu ingawa baada ya muda mchache hutoa ukweli wote. Wakati anaanza kuwa na Wema
Sepetu, Diamond alikanusha kila wakati, hata hivyo baadaye alikuwa wazi.
Na alipoachana naye na kuanza uhusiano na binti Mwigelo,
alikuwa akifanya siri hadi pale alipokuwa wazi, ingawa uhusiano wake haukudumu
sana. Kwa kiasi kikubwa, Diamond amekuwa akiibua maswali mengi kutoka kwa wadau
wake wakitaka kujua kuwa kama ataendelea kuwavua nguo akina dada hadi wakati
gani?
Uhusiano wake mpya na VJ Penny, utachukua muda gani kwa
msanii huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali, vile Mbagala, Kesho, Kamwambie,
Nataka Kulewa na nyinginezo zinazofanya vyema katika vituo vya redio na
televisheni.
No comments:
Post a Comment