Marehemu Askofu Thomas Laizer, enzi za uhai wake.
Na Kido Jembe, Dar es Salaam
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini, Askofu Thomas Laizer amefariki Dunia Alasiri ya jana, katika Hospitali ya Rufaa ya Selelian ya Mjini Arusha na kuhuzunisha wengi.
Februari 6, 2013 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alimtembelea na kumjulia hali Askofu Thomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati.

Taarifa zilipasha kuwa Askofu Laizer
alilazwa Hospitalini hapo kwa zaidi ya mwezi mmoja, na hakuna daktari wala
ndugu aliye tayari kusema ugonjwa unaomsibu.
Pinda alikwenda hospitalini hapo jana saa
9 alasiri na kukaa zaidi ya nusu saa, huku waandishi wa habari wakizuiwa
kuingia katika chumba alimolazwa cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Hata hivyo, baada ya kutoka katika chumba
hicho kama ilivyo ada ya viongozi kuzungumzia
hali ya mgonjwa, Pinda hakuzungumza na waandishi wa habari na kulikuwa na
ulinzi mkali ambapo pia waandishi wa habari walizuiwa kuzungumza naye.
No comments:
Post a Comment