Na Egbart Jeremy, Nyasa
Mvua mkubwa iliyonyesha mapema mwezi huu imesababisha baadhi
ya miundombinu kuharibiwa. Miongoni mwa maeneo yaliyoharibiwa kabisa ni Daraja
la Mbaha, na barabaraba ya Lituhi kwenda Mbamba kwa ujumla, ambapo imejifunga
kutokana na kukosekana kwa vivuko vingine.
Moja ya maeneo yaliyoharibiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Nyasa |
Mvua hiyo imechangia kwa kiasi
kikubwa ukosefu wa mawasiliano baadhi ya vijiji hadi vijiji katika mwambao wa
ziwa Nyasa. Sio madaraja pekee, bali ukuna uharibifu mkubwa sana vyanzo vya
miradi ya maji hususani katika kijiji cha Lundu.
Hadi sasa hali haijatengemaa
kiasi amabcho wakazi wa maeneo yaliyokumbwa na uharifu wanakosa huduma muhimu
kutokana na ukosefu wa usafiri kutoka eneo moja kwenda jingine. Ikumbukwe
miradi ya maji katika kijiji cha Lundu ni moja ya miradi mipya iliyokamilishwa
mapema mwishoni mwa mwaka jana hivyo kuleta nafuu kwa wakazi wake.
Lakini kutokana
na uharibifu uliotokana na mvua kubwa kunyesha utalazimisha miradi hiyo kuanza
kukarabatiwa upya.
No comments:
Post a Comment