Muhingo Rweyemamu, kulia akizungumza na simu, wakati anabadilishana mawazo na Benny Mhina, jana.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amesema kwamba
tatizo kubwa linalowasumbua wananchi wake hawajui matumizi bora ya ardhi jambo
ambalo wao kama serikali wanajitahidi kuwafikishia ujumbe wa kuwaelimisha.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa New Habari 2006 Ltd, Sinza.
DC Rweyemamu aliyasema hayo na Handeni Kwetu jana jijini Dar
es Salaam, akizungumzia kuwa pamoja na mambo mengine, lakini juu ya matumizi
bora ya ardhi yanasababisha pia muingiliano mbaya na kilimo kisichokuwa na
tija.
Alisema kwamba ofisi yake imejipanga kwa mwaka huu kueneza
elimu kwa wananchi wake, hasa juu ya matumizi bora ya ardhi, sambamba kwa
kuipima, ikiwa ndio njia rahisi ya kujitambua na kufahamu juhudi za maendeleo.
“Handeni yenye vijiji 112, asilimia kubwa ardhi yake
haijapimwa na wananchi wake hawajui namna ya kuitumia au kuiwekeza, ndio maana
migogoro imekuwa mingi kwa wilaya yangu.
“Hili najitahidi pamoja na kushirikiana na viongozi wangu
kuanzia vijiji, kata, bila kusahau Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, chini ya RC Chiku
Gallawa, ambaye amekuwa akifanya ziara mbalimbali kujionea mazingira mazima ya
maeneo yetu,” alisema.
Utendaji kazi wa Rweyemamu katika wilaya hiyo unaleta matumaini makubwa kwa wananchi wa Handeni, hasa kwa kupambana katika sekta elimu, kilimo pamoja na kuwabana wawekezaji wanaokata mkaa bila kufuata taratibu.
No comments:
Post a Comment