Picha hii imewekwa kama sehemu ya kumuwakilisha Katibu wa CCM, wilayani Mbogwe, Augustine Mbogo, ambaye picha yake tunafanya mpango wa kuipata.
Na Mwandishi Wetu, Geita
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kwa kupitia Katibu wake wa wilaya
ya Mbogwe, mkoani Geita, imewajia juu baadhi ya wanasiasa kutoka Upinzani, kwa
madai kuwa wameanzisha hoja ya kuchinja inayoendelea kuitafuna nchi kwa sasa,
hasa kwa leo kutokea machafuko wilayani Chato, mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Katibu wake, Augustine Mbogo, ikiwa ni saa
chache baada ya kuripotiwa machafuko yaliyozuka leo, huku kadhia hiyo
ikisababishwa na hoja ya kuchinja.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Mbogo alisema kwamba tangu
mwanzo Waislamu walikuwa ndio wachinjaji kwa ajili ya kuleta maisha ya
ushirikiano kwa jamii za Kikristo na Kiislamu.
Alisema kadri siasa za maji taka zilipoanzishwa na wanasiasa
wanaotaka kuiweka nchi kubaya, hoja hiyo ilianza kufanyiwa kazi, ikiwa ni jambo
lisilokubaliwa hata kidogo.
“Mimi ni kiongozi wa CCM wilaya, lakini pia ni jamii ya Roman
Catholic, nikikuwa huku nashuhudia hata Mapadre wanavyoita jamii ya Kiislamu
kwa ajili ya kuchinja, hivyo naiomba serikali kuifanyia kazi haraka tatizo hili
linaloweza kuwagawa Watanzania na kuleta machafuko zaidi.
“Sasa leo imeibuliwa hoja hiyo na watu ambao siku zote
wanataka kuiweka Tanzania katika hatari, ndio maana kila mahali wanajaribu kuingia,
ikiwamo Ukabila, udini na nyinginezo,” alisema.
1 comment:
HII NI HATARI! Tanzania imekuwapo na wazee wetu wameishi kwa amani na hata ubaguzi huu wa kidini na kuchinja walitambua na kuheshimu dini na maagizo yake. Mimi nikiwa mmoja wao nimeishi na ndugu waislamu lakini kwa kuheshimu tumekuwa tukichinjiwa na wao ili kudumisha udugu wetu. Hii kwetu Tanzania imekuwa kama sheria zetu za kimila kwani sio lazima ziandikwe popote. Leo hiki kinatoka wapi? Siasa za majitaka zitatumaliza, Laana ya mwalimu Nyerere aliyosema tukianza kubaguana kwa misingi ya dini/kabila/ maeneo yetu basi haitaishia hapo tutamalizana. Utabiri unatimia. Eee Mungu wanaotufikisha huko waangamize na malengo yao yasitimie.
Post a Comment