Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) limemteua ofisa wake Leslie Liunda wa Tanzania, kwenda Ethiopia
kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji
leseni kwa klabu zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na
Shirikisho hilo.
Akizungumza leo na Handeni Kwetu,
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema ofisa
huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari 2 mwaka huu).
Kazi hiyo anatarajiwa kukamilisha Januari
6 mwaka huu na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.
Utekelezaji wa kazi yake hiyo
nchini Ethiopia
utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia
(EFF), Wizara ya Michezo ya nchi hiyo, viongozi wa klabu na mameneja wa viwanja
husika.
No comments:
Post a Comment