Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TIMU
ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayoikabili Azam kwenye mechi ya Kombe la
Shirikisho inatua nchini leo (Aprili 17 mwaka huu) saa 7.30 mchana kwa
ndege ya Qatar Airways.
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, msafara
wa timu hiyo wenye watu 28 kwa ajili ya mechi hiyo ya kwanza ya raundi
ya pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko
maeneo ya Kariakoo.
Wakati
Azam imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa timu ya Barrack Young
Controllers II ya Liberia kwa jumla ya mabao 2-1, AS FAR Rabat imeingia
raundi hiyo moja kwa moja kutokana na nchi hiyo kufanya vizuri kwenye
michuano ya klabu Afrika.
Timu
nyingine ambazo zimeingia raundi hiyo moja kwa moja katika Kombe la
Shirikisho kama ilivyo AS FAR Rabat ni Asec Mimosas ya Ivory Coast,
Atletico Petroleos (Angola), C.S.S. (Tunisia), DC Motema Pembe (Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Ahly Shandy (Sudan), Enppi (Misri),
Heartland (Nigeria), Ismaily (Misri), Lobi Stars (Nigeria), U.S.M. Alger
ya Algeria na Wydad Casablanca (Morocco).
No comments:
Post a Comment