Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa Kick Boxing nchini, Pendo
Njau, amesema ukimya wake unatokana na kukosa wapinzani katika mchezo huo
kutokana na kukimbiwa na mabondia wake, jambo linaloathiri ngumi za mateke.
Bondia mahiri wa kike nchini Tanzania, Pendo Njau
Akizungumza hivi karibuni kwenye Ukumbi wa
mazoezi wa bondia Japhet Kaseba, Pendo alisema kinachoendelea ni mateso kwa
mabondia wa kike hasa wale wanaotegemea mchezo huo.
Alisema mchezo huo kwa akina dada umezidi kuwa
adimu, jambo ambalo linaweza kuangusha tasnia nzima, endapo juhudi za makusudi
hazitachukuliwa kwa ajili ya kuhamasisha ngumi.
“Mimi ni bondia ambaye licha ya kuwa na malengo
makubwa ya kuwika ndani na nje ya nchi, lakini nashindwa kutimiza ndoto
kwasababu ya kukosa wanawake wenye moyo kama wangu.
“Hali hii inanifanya nione umuhimu wa kuwekeza
nje zaidi, japo najua inaweza kuchukua muda kwasababu hata hao nao huangalia
rekodi za bondia katika nchi yake kabla ya kugeukia Kimataifa,” alisema.
Pendo anatokea katika mikono ya Kaseba ambaye
baada ya kuona ushindani kwenye Kick Boxing umetoweka, aliamua kuhamia kwenye
masumbwi na kuleta upinzani wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment