https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, April 15, 2013

Twanga Pepeta yaanza kuwatia hofu wadau wao kwa Leaders kuwa kweupe



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UCHACHE wa wadau na mashabiki wa bendi ya The African Stars Twanga Pepeta katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, umeanza kutia hofu wadau wake, baada ya jana shoo yao kuhudhuriwa na watu wachache, huku Salehe Kupaza akishindwa kuwapo kwenye onyesho lao.
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka
Kupaza hakuja kwenye shoo hiyo ya bonanza la kila Jumapili kwa madai kuwa anaumwa, ingawa zipo tetesi kuwa mwanamuziki huyo tegemeo kwa Twanga Pepeta ana mpango wa kutimka mapema mwaka huu kwa ajili ya akutafuta maisha zaidi.

Vipaza sauti vyetu vilivyotegwa vilivyo katika viwanja hivyo vilinasa mazungumzo ya huruma kutoka kwa wadau haswa wa Twanga Pepeta, wakionyesha wasiwasi mkubwa kutokana na mwenendo mbovu na uchache wa mashabiki wao.

“Sehemu kama hii ilikuwa haikamatiki kutokana na watu kuwa wengi kiasi cha wengineo kutumia kujiimarisha kiuchumi kwa kuleta biashara zao mbalimbali, lakini sasa kuna haja ya kuangalia kwingine kwenye mwitikio wa watu.

“Si kila anayekuja kwenye bonanza kama hili anakuja kustarehe, wengine wapo kibiashara, sasa kama hali hii itaendelea, kuna haja wenye bendi wajipange kabla ya mambo hayajakuwa mabaya zaidi,” alisema mdau huyo kwa masikitiko makubwa.

Mbali na uchache huo, lakini Handeni Kwetu haikushindwa kuwanasa wadau mahiri wa Twanga Pepeta, wakiwamo viwanjani hapo kupata burudani, akiwamo Mathew Kawogo ama Mathew Kiongoz, Karima Chichi Mhandeni, Engi Muro Mwanamachame, Dito Mwopao na wengineo.

1 comment:

Anonymous said...

Sawa kaka; umetisha

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...