Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema
hauwezi kuifikiria mechi yao dhidi ya Simba, badala yake nguvu zao zote
wamezielekeza kwa timu ya Coastal Union ya Tanga, mechi itakayopigwa Mei Mosi,
kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto
Maneno ya Yanga yanatafsiriwa
kama tusi kwa Simba iliyoonekana dhaifu katika mzunguuko wa pili na kushindwa
kutetea ubingwa wao ulionyakuliwa na Jangwani wakiwa na mechi mbili mkononi.
Mechi ya Yanga imepangwa
kufanyika Mei Mosi, wakati ile ya Simba watacheza Mei 18 mwaka huu katika
Uwanja wa Taifa, ambapo pia itakuwa ni hitimisho ya patashika ya Ligi ya
Tanzania.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, alisema kuwa mechi yao na Simba ni
ya kawaida kama ilivyokuwa ya Coastal Union, hivyo wameiweka kwanza pembeni.
“Tunakutana na Coastal kwanza
kabla ya Simba, hivyo sioni kama akili zetu, nguvu zetu zitakuwa huko, maana tumeshakuwa
mabingwa hivyo mechi zote zilizosalia zina hadhi sawa.
“Naamini tutakapofanikiwa
kuifunga Coastal Union akili zetu zitahamia kwa Simba, ukizingatia kuwa timu
yetu ni nzuri na ina uchungu wa kumaliza ligi vizuri, hivyo hili naamini
tutafanikisha,” alisema Kizuguto.
Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu na
kupeleka shangwe na nderemo kwa wapenzi wao, huku mechi mbili zilizosalia
zikibaki kama kukamilisha ratiba tu.
No comments:
Post a Comment