https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, April 12, 2013

JKT Oljoro kuwaambia nini Yanga kesho kivumbi cha Ligi Kuu


Kesho watatukoma au vipi jamani?
Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kesho kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...