Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma
inataraiia kufanya shoo ya aina yake mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro Alhamisi
ya Aprili 25, katika Ukumbi wa Aventure, wakati Ijumaa ya Aprili 27 watakuwapo katika jijini
Arusha, katika Ukumbi wa Trip A.
Baadhi ya wakali wa FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma
Shoo hizo za mwisho wa wiki hii ni sehemu ya kuwapatia
burudani wapenzi wao wa Arusha na Moshi, huku wakiwa na lengo la kuonyesha
makali yao katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Fedha
na Utawala, Kelvin Mkinga, alisema kuwa wanamini shoo hizo zitawapatia burudani
za aina yake mashabiki wao.
Alisema wanamuziki wao wapo kwenye kiwango cha juu kwa ajili
ya kutoa burudani kamili, huku wakiamini kuwa nyimbo zao zao zitakuwa sehemu
moja ya kuwapatia ladha halisi ya Ngwasuma.
“Bendi ipo imara na mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa
inaendelea kuwa juu katika tasnia ya muziki wa dansi nchini kwa kuwatumia vyema
waimbaji wenye vipaji vya aina yake.
“Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi katika shoo zetu
hizo, ambapo ni siku mbili zenye joto la msisimko kwa wadau na wapenzi wa
muziki wa dansi wa FM Academia,” alisema.
FM Academia ipo chini ya Nyosh El Saadat, akishirikiana na
waimbaji mahiri akiwapo Patchou Mwamba, Pablo Masai na wakali wengine
wanaotingisha katika tasnia ya muziki huo nchini.
No comments:
Post a Comment