Na Mwandishi Wetu, Kenya
RAIS mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ameapishiwa
rasmi leo Aprili tisa na kufurahisha Wakenya wengi waliohudhuria kwenye sherehe
hizo pamoja na wale waliofuatilia katika vyombo vya habari.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya kuapishwa leo.
Kenyatta atakuwa rais wa awamu ya nne nchini Kenya,
takriban miaka hamsini baada ya baba yake Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa
Kenya huru.
Jakaya Kikwete alipowasili nchini hapa jana na kupokelewa kwa shangwe ambapo leo amehudhuria kuapishwa kwa Kenyatta.
Sherehe za kula kiapo zinafanyika leo Jumanne Aprili
9, huku maraisi wasiopungua kumi na tano kutoka barani Afrika na wawakilishi wa
nchi za Jumuiya ya nchi za Magharibi wamehudhuria sherehe hizo, akiwamo Jakaya
Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeshangiliwa na watu
wengi wakitambua uwepo wake.
Kikwete ambaye ni rais anayejulikana kama kipenzi cha Watanzania, ameonekana kuvutia zaidi wageni na wananchi wa Kenya waliohudhuria sherehe hizo katika Uwanja wa Moi nchini hapa.
Hata hivyo, Kenyatta na naibu wake William Ruto
wanakesi ya kujibu kwenye Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC
baada ya kuhusishwa katika vurugu za baada ya uchaguzi mwaka 2007.
Miaka mitano baada ya kushuhudia uchaguzi uliogubikwa na machafuko yaliogharimu maisha ya watu zaidi ya elfu moja, lakini kwa sasa taifa la Kenya limepiga hatuwa ya Demokrasia na Kenyatta alichaguliwa duru la kwanza tu la uchaguzi na kura ndogo zaidi ya mpinzani wake Raila Odinga kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura.
Matokeo hayo yalipingwa na mrengo wa muungano wa Cord unaongozwa na Raila Odinga na kupekeleka kesi mahakamani, kesi ambayo baada mahakama ilitupilia mbali na kumtaja Uhuru Kenyatta kama mshindi halali katika uchaguzi uliofanyika Marchi 4, na Raila Odinga kukiri kushindwa na kukubali matokeo.
Katika uchaguzi wa mwaka 2007 baada ya Raila Odinga kutangazwa kuwa ameshindwa kwenye uchaguzi na Mwai Kibaki na baaae kuzuka machafuko ya umwagaji mkubwa wa damu kuwahi kutokea katika Historia ya Kenya.
No comments:
Post a Comment