Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAREMBO wamejitokeza katika kushiriki shindano
lijalo la Redds Miss Kibaha 2013.
AKhadija Kalili, Mkurugenzi wa Linda Media Solution
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO), ambaye pia ndio Mratibu wa shindano
hilo Khadija Kalili alisema amefurahishwa na mwitikio wa warembo waliojitokeza
hadi sasa katika kuwania taji la Miss Kibaha.
“Mwitikio wa warembo kwa kweli unatia moyo hivyo kwa kuwa muda wa
kufunga milango ya kupokea warembo bado iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini
kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na
ushindani zaidi,” alisema Kalili.
Kalili aliwataja baadhi ya warembo waliojitokeza kuwa ni Nzeran
Kitano, Martina Kapaya, Asma Said, Maud Bernad, Flora Mlowola na Nancy James.
Warembo wengine ni Esther Albert, Beatrice Bahaya, Jenipher
Njabiri na Rachel John.
Warembo wa Miss Kinaha 2013 tayari wameanza mazoezi wakiwa chini
ya wakufunzi wawili ambao ni Sweet Ray na Bob Rich.
Shindano la kumsaka Miss Kibaha litafanyika katika ukumbi wa
Kontena uliopo Kibaha Maili Moja Mkoani Pwani.
Kalili aliongeza kwa kusema kuwa shindano la mwaka huu litaandika
historia mpya ya urembo mkoani humo kwakuwa Kampuni ya LIMSO imejipanga hivyo
mashabiki wa mashindano ya urembo wa Wialaya ya Kibaha na Mkoa wa Pwani kwa
ujumla wakae mkao wa kupata raha.
“Shindano la mwaka huu litakuwa la aina
yake kulinganisha na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu LIMSO
imejipanga” alijigamba Kalili.
Kalili anawataja baadhi ya wadhamini
waliojitokeza kudhamini shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC
Africa,Michuzi Blog , The African Stars Entertainment (ASET) na Redds Premium
Cold.
No comments:
Post a Comment