Jumla ya watuhumiwa watano wamekamatwa na jeshi la polisi baadhi yao wakiwa ni askari wa JWTZ kwa tuhuma za kumuua dereva wa Bajaji Yohana Cyprian mkazi wa Mbezi Beach.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela amesema kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni linatoa rai kwa wananchi na askari kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya jazba.