Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MARA kadhaa migogoro baina ya
wananchi na Serikali huweza kuchochewa na wanasiasa, Taasisi zisizo za Serikali
na za Serikali yenyewe lakini ikiwa na malengo ya kila kundi kujinufaisha
lenyewe kiuchumi, kisiasa.
Makundi kama ya NG’O hujitokeza
kwa wingi pale yanapoona sehemu yenye mgogoro ina maslahi kwao na sehemu ya
kuweka huruma mara kadhaa imekuwa ni ndogo kuliko maslahi binafsi au ya taasisi
husika.
Hali hii mara nyingi hujitokeza
hasa panapokuwa na migogoro ya ardhi baina ya wananchi na wawekezaji utakuta
NG’O zinarundikana na kuanza kuhamasisha wananchi kufanya vurugu zisizokuwa na
mantiki ya kuendeleza kijiji au sehemu husika kwa maslahi ya taifa na kijiji
chenyewe.
Kwa takribani miaka 20 sasa eneo
la Loliondo limekuwa na migogoro ya muda mrefu inayotokana na muingiliano wa
matumizi ya ardhi katika eneo lililotengwa na kutangazwa na serikali kuwa la
Pori Tengefu la Loliondo.
Hata hivyo hakuna asiyefahamu kuwa
mrundikano wa NG’O zaidi ya 30 ni kutokana na kutaka maslahi
binafsi au ya taasisi kwa kua Hifadhi ya Taifa ya Serengeti; Tarafa ya Loliondo
inajumuisha Pori Tengefu (Loliondo Game Controlled Area –LGCA) eneo ambalo
lenye vitega uchumi vingi.
Baadhi ya vitega uchumi katika eneo hilo ni la
wawekezaji wa Otterlo Business Corporation Ltd (OBC) ambao walifanikiwa kupata
kibali cha uwindaji katika hifadhi hiyo.
Thomson Safaris ambao wanaendesha shughuli zao za utalii wa asili katika maeneo ya Sukenya, Soitsambu. African Safari | Mount Kilimanjaro Climb
Dorobo Tours and Safaris ambao wanaendesha utalii wa kiikolojia.
Sokwe Asilia hawa wanaendesha kambi za kudumu za muda Nomad Safaris: Kampuni hii inamiliki kambi lakini hizi ni baadhi tu ya kampuni.
Kutokana na hali hiyo inanisukuma kusema kuwa wawekezaji hawa wako katika ushindani mkubwa ikiwa ni pamoja na kwenye maslahi kutokana na suala zima la kiutalii, mapambano katika uchumi na kila mmoja kupigania kupata eneo kubwa la Loliondo.
Kutokana na masuala hayo yote kuna kila sababu
ya hawa washindani kuwatumia wanasiasa katika kuhakikisha kuwa wanalinda
maslahi yao binafsi na hata kuwatumia viongozi wa vijiji na wananchi ili
kila mmoja aweze kuvutia kwake kwani waswahili wanasema kila mwamba ngoma
huvutia kwake na hivyo ndivyo ilivyo kwa mgogoro huu wa Loliondo eneo ambalo
lina vivutio vizuri vya kiutalii.
Loliondo imekuwa ni sehemu ya
mgogoro mkubwa ambao umekuwa ukiundiwa tume kwa takriban mara mbili mfululizo
inakua na majibu lakini hatua madhubuti ya kuunusuru mgogoro huo kutochukuliwa
na hii husababisha kadhia na vurugu kuchukua nafasi yake.
Katika taarifa ya tume ya
uchunguzi ya mwaka 2009 iligundua kuwa NGOS zisizo za Serikali kuwa ndio sababu
kubwa ya kueneza chuki na hata kusababisha mapigano baina ya wananchi na
kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Ortello Business Cooperation (OBC) ya Falme
za Kiarabu (UAE).
Lakini kutokana na hali ya mgogoro
kuendelea Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki aliona
ni vyema kuweza kuufanyia utatuzi wa haraka ili wananchi waweze kuishi kwa
amani na furaha huku wakifurahia matunda ya wawekezaji wao.
Waziri alifanya ziara katika eneo
hilo kwa takribani mara tatu kuzungumza na wananchi na mwekezaji wa OBC
ili kujua chanzo na kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Hata hivyo katika hali isiyo ya
kawaida wanasiasa ,NGO wamekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha wanaweza
kuingilia majadiliano hayo ya amani kwa maslahi yao na si kwa maslahi ya
Wananchi.
MAJIBU YA ZIARA YA WAZIRI LOLIONDO
Hata hivyo katika ziara zake hizo
naye amegundua kuwa wanasiasa wamekuwa katika mstari wa mbele kuhamasisha
vurugu kutokana na kulinda mtaji wa kura 2015 jambo ambalo alisema si sahihi na
kwamba halitakiwi kufumbiwa macho hata kidogo.
Anasema migogoro iliyopo
Loliondo imejenga hisia zisizo sahihi kwa watanzania na hata wengine
katika jumuiya za Kimataifa na ilikua vema kupata ufumbuzi wa kudumu wa
migogoro ya ardhi katika eneno hilo.
Hata hivyo anasema kuwa ili
kunusuru ikolojia ya Hifadhi za Serengeti ,Ngorongoro na pori Tengefu
Loliondo, Serikali itatenga sehemu ya ardhi ya pori tengefu la Loliondo yenye
ukubwa wa Kilomita za mraba 1,500 kutoka kwenye eneo la kilomita za mraba 4,000
za pori hilo itakayoendelea kuwa na hadhi ya pori tengefu kwa ajili ya
kulinda mazalia ya wanyamapori,mapito na vyanzo vya maji kwa ajili
ya ustawi wa hifadhi hizi kwa manufaa ya wananchi wenyewe na taifa kwa
ujumla.
“Serikali itasimamia eneo
litakalobaki kuwa pori tengefu kwa mujibu wa sheria za uhifadhi wa wanayamapori
na ardhi itakayobaki baada ya kuondoa eneo la pori Tengefu Loliondo itasimamiwa
na vijiji kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya kijiji namba 5 ya mwaka
1999,”anasema Kagasheki.
Anasema baada ya hapo wananchi
watawezeshwa kuanzisha eneo la jumuiya la hifadhi ya wanaymapori (WMA) katika
ardhi itakayobaki kuwa ardhi ya kijiji kwa mujibu wa sheria ya ardhi .
Nasema pia mipango ya matumizi
bora ya ardhi ya vijiji katika eneo la Loliondo utaandaliwa na utaambatana na
huduma za mifugo ndani ya vijiji,kwa mfano wa majosho ,malambo ya maji ya
mifugo ,minada na mengineyo.
Alisisitza kuwa msisitizo wa
serikali ni kuwataka wafugaji kufuga kisasa zaidi kufuga mifugo inayoendana na
ukubwa wa eneo la malisho lililopo katika kijiji husika ambapo sheria ya
kudhibiti idadi ya mifugo itakayoruhusiwa kwa mujibu wa uwezo wa eneo la
malisho kumudu itazingatiwa ili mifugo isizidi kwenye eneo husika pia.
Hata hivyo kulikuwa na tamko
ambalo lilitolewa na wananchi ,viongozi wa kisisa na wanaharakati kwa serikali
halikuwa sahihi lakini pia imeona kuna haja ya kuangalia upya eneo alilopewa
mwekezaji OBC na hata ikibidi kupunguizwa ili wananchi wapate maeneo hayo.
Waziri Kagasheki pia aliwataka
wananchi kutii sheria bila shuruti kuondoka katika maeneo tengufu huku akisema
kwa sasa hakuna kubembelezana ni wakati wa kufuata sheria.
Lakini alifika mbali zaidi na
kuzishangaa NGO mbalimbali ambazo anasema zafikia 30 kujiweka katika eneo hilo
kwa ajili ya kuchochea vurugu kwa maslahi yao na si ya wananchi.
Kutokana na hali hiyo alizitaka
NGO kuachaa kuchochea wananchi vurugu na badala yake kuhamasisha amani na
uwasaidia wananchi njia mbadala za kupata maendeleo.
Lakini pia anashangazwa na kitendo
cha eneo kubwa la Loliondo kukaliwa na kuendeshwa shughuli zake na kabila la
watu wa kimaasai ambao ni wafugaji na ndio ambao wamekuwa pia kichocheo kikubwa
cha vurugu hizo.
“Hii haikubaliki hata ,hivi kwa
mfano ingetokea wafugaji wakitanzania wangejaa kule Kenya wale wangekubali
sidhani kama watakubali na hii inatokana na Kenya kuwa na uhaba mkubwa wa
ardhi, lakini si vizuri kuwabagua ila wasianzishe vurugu kwa maslahi yao huku
wakijua wanaloliondo wanategemea watalii katika kukuza uchumi pia,”anasema
Kagasheki.
Vyombo mbalimbali vya habari
vilikariri uongozi wa
Kampuni ya Ortello Business Corporation (OBC),kwa kusema kuwa maslahi
binafsi yakiwemo ya wanasiasa na baadhi ya watendaji serikalini, ndiyo chanzo
cha mgogoro unaoendelea katika eneo tengefu la ardhi la Loliondo ambako kampuni
hiyo imepewa kibali cha kuwinda.
Mkurugenzi wa OBC Tanzania, Isaac Mollel, amesema, maslahi hayo binafsi yanachangia kuwepo kwa mgogoro huo, lakini kama sheria zikifuatwa, hakutakuwa na mgogoro katika eneo hilo ambalo Ortello imekuwa ikiendesha shughuli zake kwa kibali cha serikali tangu mwaka 1993.
Mollel anaungana na kauli ya Waziri Kagasheki na kusema kuwa mgogoro huo hutokea pindi Serikali inapotaka kugawa vitalu na kila watanzania wakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu, akitolea mfano wa mwaka 1993 na sasa watu wanapolekea uchaguzi wa mwaka 2015 .
Anasema,kwa kuwa Kenya ardhi ni tatizo, wapo baadhi ya watu kutoka nchi hiyo ambao wengi ni wa jamii ya wafugaji wa Kimasai, wameingia Loliondo na kuchukua ardhi, na kusababisha mtafaruku kwa jamii ya wenyeji.
Mkurugenzi wa OBC Tanzania, Isaac Mollel, amesema, maslahi hayo binafsi yanachangia kuwepo kwa mgogoro huo, lakini kama sheria zikifuatwa, hakutakuwa na mgogoro katika eneo hilo ambalo Ortello imekuwa ikiendesha shughuli zake kwa kibali cha serikali tangu mwaka 1993.
Mollel anaungana na kauli ya Waziri Kagasheki na kusema kuwa mgogoro huo hutokea pindi Serikali inapotaka kugawa vitalu na kila watanzania wakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu, akitolea mfano wa mwaka 1993 na sasa watu wanapolekea uchaguzi wa mwaka 2015 .
Anasema,kwa kuwa Kenya ardhi ni tatizo, wapo baadhi ya watu kutoka nchi hiyo ambao wengi ni wa jamii ya wafugaji wa Kimasai, wameingia Loliondo na kuchukua ardhi, na kusababisha mtafaruku kwa jamii ya wenyeji.
No comments:
Post a Comment