Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
|
WASANII chipukizi 300 kutoka
vikundi 15 jijini Dar es Salaam wamejitokeza kushiriki maonesho ya kukuza
vipaji yaliyoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Jumamosi ya
Aprili 27 katika ukumbi wa hoteli ya StarLight, Mnazi Mmoja Dar es Salaam, ikiwa ni mipango ya kukuza na kuendeleza sanaa.
Msemaji wa SHIWATA, Peter Mwenda
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Msemaji wa SHIWATA, Peter Mwenda, alisema kuwa vikundi ambavyo
vimethibitisha kushiriki pamoja na Kaole Sanaa Group, Splendid, Uyoga Boga na
vingine katika fani ya Bongo Flava, Taarab, Maigizo, Ngoma, Mazingaombwe, Sanaa
za Ufundi, Kung Fu, Sarakasi, Kusheki, Kwaya na Ngonjera.
Maonesho kama haya yatafanyika
kila mwezi na kiingilio ni bure na vikundi vingine ni Super Shine Morden
Taarab,Zijiu,Edeneza Brass Band,Asili Africa,Mege Arts,Kintu,Army
Kwanza,Wachapakazi,Tanhope,Tanz Arts,Mshikamano,Big House,Lutenga
Boys,Kilimasta,Manuary.
Madhumuni makubwa ya tamasha hilo
ni kuibua vipaji vya wasanii chipukizi ili kazi zao ziweze kupata soko hivyo
mapromota, Majd,Maproducer wa filamu wasikoke kufika katika maonesho hayo ili
kuona mastaa chipukizi ambao ambavyo vipaji vyao bado havijaonekana.
“Vijana wa sanaa mbalimbali
wanatakiwa kufika katika ofisi za SHIWATA zilizopo Bungoni Ilala ili kujisajili
kwa ajili ya maonesho mengine yanayofuata.
“Tanzania kuna wasanii wengi wenye
vipaji lakini kazi zao hazisikiki wala kuonekana kwenye vyombo vya habari hivyo
hiyo ni fursa kutumia maonesho hayo kama soko la kazi zao katika jiji la Dar es
Salaam,” alisema.
Wasanii mbalimbali ambao vipaji
vyao vitakubalika sokoni watanufaika kupata ajira ya kuuza kazi zao pamoja na
kushiriki katika matamasha mbalimbali ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment