Oscar Shelukindo akicheza pool table
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupiti
bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kudhamini mashindano ya mchezo wa
Pool Table kwa vyuo vya elimu ya juu ambayo yataanza Mei 4, mwaka huu.
Mashindano hayo yanajulikana kama
“Safari Lager Higher Learning Pool Championships” yanafanyika kwa mwaka wa nne
sasa na Safari Lager imekuwa wadhamini wakuu kwa miaka yote na bingwa katika
mkoa atapata 500,000, wa pili 300,000 na 200,000 na mshindi kwa ngazi ya taifa
atapata kikombe pamoja na 2,500,000.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana meneja wa bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo
alisema nia ya kudhamini mashindano haya ni kuhamasisha wanavyuo kucheza mchezo
wa pool table ikiwa ni burudani baada ya shughuli za masomo yao.
Pia alisema michezo ni muhimu kwani
hupumzisha akili na kufanya warudi darasani wakiwa na ari mpya na pia
hukutanisha na watu mbalimbali.
“Michezo mingi hasa pool ni burudani na
husaidia akili kupumzika baada ya masomo na kufanya akili kufikiri upya na kwa
ubunifu na husaidia kuwakutanisha na watu mbalimbali pia husaidia vijana
watumie muda wao vizuri badala ya kujiunga na magenge yanayoweza kupotosha
maadili”, alisema Shelukindo.
Naye Katibu wa chama cha Pool Tanzania
(TAPA) Amos Kafwinga alisema kuwa mashindano haya yataanzia kwa vyuo kushindana
katika ngazi ya mkoa na baadae mikoa yote itashindana katika ngazi ya mikoa na
baadae katika ngazi ya Taifa ili kupata mshindi wa jumla kwa vyuo vyote.
Pia alisema mashindano ya mwaka huu
yatahusisha vyuo vikuu vilivyo katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya,
Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam na jumla ya vyuo 54 vinategemewa
kushiriki
Bingwa mtetezi ni Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustino (SAUT) cha jijini Mwanza ambao waalichukua ubingwa kwenye
fainali zilizofanyika Iringa mwaka jana na fainali za mwaka huu
zitafanyikajijini Dar es Salaam mwanzoni mwa Juni mwaka huu.
|
No comments:
Post a Comment