Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Extra
Bongo, Next Level, Ally Choki, amesema kwamba yupo kwenye mikakati ya
kuwanyakua na kuwatambulisha waimbaji wasiozidi watatu kwa ajili ya kuimarisha zaidi safu
yao.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki
Extra Bongo imezidi kuteka
nyoyo za wapenzi wao, huku shoo zao zikipendwa na watu wengi katika kumbi
mbalimbali za starehe nchini.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Choki alisema kwamba anaamini kufanikiwa kuwapata waimbaji wao mambo
yao yatakuwa mazuri katika hali ya kujiweka sawa kiushindani.
Alisema ingawa kwa sasa bendi
yao ipo juu kimuziki, lakini bado wanahitajika wa kuleta ushindani kwa
kuhakikisha kuwa waimbaji wenye vipaji na uwezo wa juu wanaingia katika bendi
yao.
“Huu ni wakati wa kuhakikisha
kuwa Extra Bongo inazidi kuwika katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa, hivyo
naamini endapo tutafanikiwa kuwanasa waimbaji hao wawili au watatu, kila kitu
kitakuwa sawa.
“Sisi ni watu wa kazi si wa
kupiga porojo, hivyo jukumu letu kwa sasa ni kuendelea na mazungumzo na hao
ambao tumewaomba tuwe nao katika kuimarisha bendi yetu ya Wazee wa Kizigo,”
alisema.
Bendi hiyo kwa sasa imesheheni
waimbaji wenye uwezo wa kutisha, akiwamo Ramadhan Masanja Banza Stone, Rogati
Hega Katapila, Khadija Kimobiteli Athanas na wengineo.
No comments:
Post a Comment