Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
LIGI Darajala la Pili Mkoa wa Dar es Salaam , hatua ya sita
bora imezidi kushika kasi ambapo hadi sasa timu ya Red Coast inaongoza ligi
hiyo kwa kujikusanyia pointi 7 baada ya kucheza mechi tatu.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam, Mohamed Mharizo, Red Coast imejikusanyia pointi hizo baada ya
kuzifunga Abajalo bao 1-0, huku ikilazimishwa sare ya bila kufungana na
Friends Rangers na jana Jumatatu iliichapa Sharif mabao 3-1, katika mechi
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Airwing.
Friends Rangers wanashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi
5, ilizozivuna kwa kutoka sare ya bila kufungana na Day Break katika mechi ya
kwanza, kasha kulazimishwa tena sare ya
bila kufungana na Red Coast na jana
Jumatau iliifunga Boom FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa.
Abajao inashiaka nafasi ya tatu ikiwa na pointi 4, huku Sharif
Star ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 3, ikifuatiwa na Day Break yenye
pointi 3 wakati Boom FC ikiburuza mkia kwa kuwa na pointi 1.
Kesho Jumatano ligi itaendelea kwa michezo mitatu, Abajalo
vs Friends Rangers uwanja wa Kinesi, Red Coast vs Boom uwanja wa Makurumla na
Sharif Stars vs Day Break uwanja wa Airwing, huku Ligi hiyo ikitarajiwa kumalizika
Aprili 27 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment