Na Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF),
awametaka wananchi wa mkoa wake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika
shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Mbunge
Mwidau akisalimia na wanawake wa kikundi cha wajasiriamali wafugaji wa kuku wa
Kata ya Pongwe kijiji cha Marizara.
Mbunge
wa Mwidau, akikagua madarasa ya shule ya Sekonadari ya Msambweni, kulia ni
Diwani wa Kata ya Msambweni Abdulrahaman Hassan (CUF).
Mbunge
Mwidau akikabidhi mifuko kumi ya saruji kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Msambweni
Bahati Marungu kwa ajili ya ujenzi shule ya Sekondari ya Kata ya Msambweni.
Mbunge
wa viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akipata maelezo ya mradi wa kisima
cha maji kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mwera Maisha Mkaidi (CUF), wengine ni
baadhi ya viongozi na wananchi wa kata hiyo.
Mbunge
Mwidau, akikabidhi fedha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi Jamali Nassoro
kwa ajili ya kununua mifuko kumi ya saruji ikiwa ni sehemu ya ahadi ya mbunge
katika kuunga mkono ujenzi wa shule ya Msingi Kipumbwi Pwani.
Kauli hiyo aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza
katika ziara yake hiyo katika kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya
Pangani, ambapo alisema ni muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu wake.
“Suala la amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa
kampeni za uchaguzi, ni jukumu letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha
tunashiriki katika miradi ya maendeleo kwa dhati.
“Ni
wazi Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi wetu
hasa baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana na kutokuwepo na
usimamizi mzuri. Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni wazi tutafanikiwa kufikia
lengo letu,” alisema Mwidau.
Alisema kutokana na hali hiyo kila mara
amekuwa akishiriki katika kuhamasisha maendeleo katika maeneo yote ya mkoa huo
bila kujali uongozi wa kaa upo chini ya chama cha CUF au CCM.
“Tanga tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu
ya kujivunia jambo hili
ingawa kukosekana kwa usimamizi madhubuti kwetu imekuwa ni kilio kikubwa kwa
wananchi wetu tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa huu tuna wajibu wa
kuliangalia hili,” alisema Mbunge Mwidau.
Katika ziara hiyo akiwa
wilayani Pangani Mwidau, alisema kuwa amefurahishwa kuona wananchi na viongozi
wa Serikali ya Kijiji cha Mwera kuamua kuchimba kisima kikubwa zaidi ya
kilichopo sasa na katika hilo amefurahishwa kuona mchango wa awali wa mashine
aliyoitoa imewezesha kujengwa kwa kisima kisima kingine kikubwa cha futi 45 na
kipenyo cha nchi sita.
No comments:
Post a Comment