Askofu wa kituo cha maombezi na uponaji cha Overcomers Power
Center (OPC) Dkt Boaz Sollo (kushoto) akimakabidhi tuzo ya heshima
mfano wa ramani ya Tanzania waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
jana katika hafla ya kuchangia ujenzi wa kanisa na kuendeleza kituo cha
radio Overcomers Fm, katika harambee hiyo Lowassa aliahidi kuachangia
milioni 15 na kufanikisha kupata Tsh zaidi ya milioni 75 zikiwemo
fedha taslimu na ahadi picha na Francis Godwin.
Na Francis Godwin, Iringa
WAZIRI
mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema kuwa mbali ya kuwa yeye si
tajiri ila bado ataendelea kufanya kazi yake kwa ukaribu zaidi na
jamii ikiwa ni pamoja na kushirikiana na marafiki zake kusaidia na
kuwataka wale wote wenye kusema dhidi yake kuendelea kusema ila
hatarudi nyuma katika kutoa misaada kama njia ya kutafuta baraka za
Mungu.
Lowassa
ambae pia alikabidhiwa tuzo ya heshima kwa ajili ya kuendeleza
kulipigania Taifa la Tanzania ,huku mwenyewe akichangia kiasi cha Tsh
milioni 15 na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akichangia
milioni 9 kati ya fedha zote zaidi ya Tsh milioni 75 zilizochangwa
kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa kanisa la OPC mkoani Iringa kama
njia ya kuhamasisha amani katika Taifa ametaka watanzania kuwapuuza
wale wote wanaoeneza siasa za uchochezi .
“Nataka
kuwaomba leo wachukieni wachochezi na pia niwaelezeni kuwa mimi si
tajiri ila nina utajiri wa watu na ushawishi na ninafanya mambo haya
ili kumbukumbu yangu iweze kuandikwa Mbinguni na nimekuwa
nikialika watu wengi na nimekuwa nikifika wacha wenye kusema
waseme watasema ila usiku watalala wenyewe ….sitaacha kusaidia kwa
kuogopa kusemwa”
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyoandaliwa na kituo cha maombezi na uponyaji
mkoani Iringa Overcomers Power Center (OPC) na kufanyika katika ukumbi
wa St Dominic mjini Iringa leo Lowassa alisema kuwa yeye si tajiri
kama ambavyo watu wanavyofikiri ila amekuwa akipewa nguvu na rafiki
zake ambao wamekuwa wakimuunga mkono pindi anapoalikwa katika hafla
mbali mbali.
“Nataka
kwanza kuwashukuru ndugu zangu wa mkoa wa Iringa na napenda
kumshukuru zaidi Askofu Dkt Boaz Sollo kwa kunialika mkoani Iringa
…..ila napenda kuwaeleza kuwa si kwamba nachangia michango mbali
mbali katika jamii kama mimi ni tajiri ila mimi ni mtumishi nisiye na
faida na nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu.
Pia nawashukuru
sana wabunge wenzangu ambao wamepata kushiriki name leo katika
ziara hiyo akiwemo mbunge machachari bungeni Deo Filikunjombe ,
Kagi Lugola na dada yangu Ritta Kabati bila kumsahau mbunge Mendradi
Kigola kwa kuungana nami leo naamini nao wamepanda mbegu bora”.
Lowassa
alisema kuwa anatambua bado ana mialiko migi sana na lazima
anaifanyia kazi mialiko yote kama ambavyo jamii imepata kumwalika na
kuwa hata hatua ya mkoa wa Iringa kumpa tuzo hainamanishi kuwa ni
mwisho wa yeye kualikwa.
Hata
hivyo Lowassa alisema kuwa kwa upande wake anapongeza jitihada
za askofu Dkt Sollo kwa kuwa na mipango na mitazamo ya kulisaidia
Taifa kwa kuanzisha ujenzi wa kanisa kwa ajili ya kudumisha amani na
kwenda mbali zaidi kwa kuanzisha kituo cha radio Overcomers Fm
chambo ambacho kitatumika kudumisha amani ya mkoa wa Iringa na Taifa
pia
Kuhusu
amani ya Taifa la Tanzania LOwassa alisema kuwa alikuwa ni miongoni
mwa watu walioalikwa Kenya katika sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa
Kenya Uhuru Kenyatta ila sehemu kubwa ya wote waliotoa salam zao
walitumia muda mwingi kupongeza vyombo vya habari kwa kulinda amani na
hivyo kuvitaka vyombo vya habari za Tanzania na wanahabari kuendelea
kuandika habari bila kuhatarisha amani ya Taifa
“Tusiruhusi
amani ya nchi yetu iyumbishwe na mtu awaye yeyote na kila
mtanzania anapaswa kulinda amani hii kwa nguvu zote ….Nawaombeni
wanahabari tunzeni amani yetu…wapuuzeni wale wote wanaoch0chea
machafuko katika Taifa hili ….tuachane na udini wala ukabila katika
taifa letu ila “
Katika
hatua nyingine Lowassa aliwapongeza wabunge wa CCM ambao
wameendelea kupigania wanyonge bungeni akiwemo Deo Filikunjombe
mbunge wa Ludewa na mbunge wa jimbo la Mwibara Kagi Lugola kuwa ni
miongoni mwa wabunge ambao amekuwa akiwapenda kutokana na kusema kweli
bungeni.
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe alisema kuwa mbali ya kutoa ahadi ya
kuchangia kiasi cha Tsh milioni 9 ila bado atamwalika Lowassa
jimboni kwake Ludewa na kuwa kanisa hilo la OPC halijakosea kumpa
tuzo ambayo ni ramani ya Tanzania kutokana na Lowassa kuwa ni mtu wa
watu mpendwa na watu na kuwa tuzo hiyo ina maana kubwa na hawajakupa
ramani ya jimboni kwako Monduli
Filikunjombe
alimtaka Lowassa kuendelea kuchapa kazi na kuwa hajakosea
kuwaalika wao kwani bungeni kuna wabunge zaidi ya 300 ina
amewachagua wao pekee ni jambo la kumshukuru na kumfananisha L0wassa
na mti unaopigwa mawe kuwa ni mti wenye matunda.
“Nakuomba
Lowassa simama Imara sisi wana Iringa tupo nyuma yako na niseme
tuna kazi kubwa ya kuifanya katika Taifa hili kubwa ni kumwomba Mungu
na makanisa na dini zote kuungana katika maombi zaidi kwani vita ni
kubwa mbele," alisema.
Kwa
upande askofu Dkt Sollo mbali ya kumpongeza Lowassa bado alisema
kuwa wao kama kanisa wataendelea kumwombea afya njema na kuona kuwa
mambo yake yanafanikiwa na ndio maana ya kumpa tuzo hiyo ya heshima.
Sollo
alisema kuwa mchango wa TSh milioni 15 ulioahidiwa na Lowassa na ule
wa milioni 9 ulioahidiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe ni mchango ambao wao wanaupongeza na kuwapongeza wabunge
wengine akiwemo Ritta Kabati aliyeahidi Tsh milioni 2 ,Benki ya
wananchi Mufindi milioni 2 , mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu milioni 2 mfanyabiashara Salim Abri milioni 1 na wengine
wengi ambao wamepelekea kupata zaidi ya Tsh milioni zaidi ya 75
pesa taslim na ahadi.
No comments:
Post a Comment