https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, April 08, 2013

Maandalizi Ruaha Marathon mkoani Iringa yapamba moto


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MRATIBU wa mashindano ya riadha ya Ruaha Marathon, Albert Sanga, amesema kwamba wanaendelea na maandalizi yao kwa ajili ya kufanyika kwa mashindano hayo kwa ufanisi na kukutanisha watu zaidi ya 2500 mkoani Iringa, hapo Mei 25.
Ruaha Marathon yamepangwa kutimua vumbi mkoani Iringa, huku wanariadha kutoka ndani na nje yaa nchi wakitarajiwa kuonyeshana uwezo huku dhima kubwa ya mashindano hayo ikiwa ni kukuza sekta ya utalii wa ndani hapa nchini.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka mkoani Iringa, Sanga alisema kwamba wamekuwa wakifanya juhudi za hapa pale ikiwa ni kuwasiliana na wadau namna ya kuandaa mashindano yenye mguso na malengo makubwa kwa sekta ya riadha.

Alisema kuwa Ruaha Marathon ni kwa ajili ya Watanzania wote, huku lengo lingine ni kukusanya fedha za kuwasaidia watoto walemavu, hivyo wanaamini wakifanikisha mbio hizo kila sekta itafanikisha, sambamba na kukuza utalii.

“Ruaha Marathon tunataraiia kushirikisha watu kutoka Italia, Canada, Marekani, Uingereza, Australia, Kenya, Ethiopia, Afrika Kusini na nchi nyingine, hivyo kwasababu hii lazima waandaaji tupigane kadri ya uwezo wetu kwa ajili ya kufanikisha lengo letu.

 “Naamini mambo yatakuwa mazuri kwa kuona kuwa tunafanikisha mashindano haya kwa kiwango cha juu na kuendeleza sekta ya michezo pamoja na kutangaza utalii wetu ambao kwa hakika utakuwa na tija kwa namna moja ama nyingine,” alisema.

Kwa mujibu wa Sanga, watu wa kada mbalimbali, wakiwamo mawaziri, wabunge na wengineo nao watakuwapo kwenye mashindano hayo kuangalia kila kitakachojiri kwa siku hiyo maalum ya Ruaha Marathon mkoani Iringa.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...