CHAMA cha Soka
wilayani Korogwe (KRFA), kimewataka waamuzi wao wachezeshe kwa haki Ligi ya
Gambo Cup inayoendelea, ili kuondoa malumbano na kupatikana mshindi wa haki
kwenye michuano hiyo na hatimae kukuza kiwango cha michezo wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya Korogwe, Mrisho Gambo na mdhamini wa Gambo Cup wilayani humo.
Mashindano hayo
yanayoendelea wilayani Korogwe yamepangwa katika vituo nane, huku yakiandeshwa
kwa udhamini wa Mkuu wa Wilaya Korogwe, Mrisho Gambo.
Akizungumza kwa njia
ya simu, Mwenyekiti wa Chama hicho, Peter Juma, alisema kuwa kitendo cha kuwabana
waamuzi wao kimetokana na kuhitaji ufanisi katika mashindano yao.
Alisema katika
mashindano yoyote ya mpira wa miguu, waamuzi wana nafasi kubwa ya kuharibu au
kujenga, hivyo wamejitahidi kuwaelimisha namna gani wanatakiwa wachezeshe kwa
kufuata sheria za soka zilizopangwa.
“Tumekuwa
tukizungumza na waamuzi mara kwa mara katika hali ya kuwajulisha namna gani wao
ni muhimu na hawapaswi kuchezesha kwa matakwa ya watu fulani.
“Tunahitaji maendeleo
ya michezo hasa mpira wa miguu, hivyo naamini tutafikia hatua nzuri na kuiweka
wilaya yetu katika nafasi nzuri katika kiwango cha michezo,” alisema Juma.
Baadhi ya waamuzi wa
soka nchini wamekuwa wakichezesha mechi huku wakilalamikiwa kuwa wanazindamiza
baadhi ya timu, jambo linalosababisha Shirikisho la Soka nchini TFF kupiga
kelele kuwakemea waamuzi hao.
No comments:
Post a Comment