Na
Mwandishi Wetu, Tanga
MWENYEKITI
wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mkoa wa Tanga ni
moja kati ya mikoa maarufu kwa viwanda nchini lakini hivi saa hali ya kimaendeleo
katika mkoa huo imekuwa mbaya.
Kauli
hiyo ameitoa leo mjini hapa alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu maendeleo ya
uchumi kwa Mkoa wa Tanga katika kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wananchi
(CUF) kwa kushirikiana Taasisi ya Maendeleo ya demokrasi kwa vyama vya siasa ya
nchini Denmark (DIPD).
Profesa Lipumba
Profesa
Lipumba alisema kuwa hakuna haki bila kuwa na maendeleo yanamgusa
mwananchi wa kawaida.
Alisema
Mkoa wa Tanga umefanikiwa kuwa na rasimali nyingi ikiwemo zao la Mkonge ambalo
kwa sasa limekosa msukomo hali inayochangia umaskini kwa wananchi wa mkoa huo.
"Pamoja
na Tanga kuwa na fursa nyingi za kiuchumi lakini bado kadri siku zinavyokwenda
umaskini umekuwa ukiwatesa wananchi. Viwanda vilikuwa zaidi ya 70 lakini sasa
hakuna hata kimoja kinachofanya kazi huku zao la mkonge lilikosa msukumo wa
makusudi kwa wananchi wake.
"Katika
soko la dunia inaonyesha kuwa Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa mwaka
lakini sasa mkonge umeporomoka na kufikia tani 25,000 tu hali ambayo imekuwa
ikiongeza umaskini kila kukicha. Kama kungekuwa na msukumo wa makusudi wa
kufufu zao hili ni wazi Tanga ingekuwa imepaa kimaendelo kwa wananchi wake
kutokana na kuwa na kila aina ya rasilimali zikiwemo za matunda na
mbogamboga," alisema Profesa Lipumba
Profesa
Lipumba, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi duniani, alisema ili kuweza
kufikia malengo ya mkoa huo kuweza kupambana na umaskini ni lazima serikali
ikubali kwa kufanya uwekezaji hasa katika kufungua bandari ya Tanga ambayo ni
lango kuu la kiuchumi.
Alisema Bandari ya Tanga imekuwa haitumiki ipasavyo hali
inawechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa umaskini na hazorotesha harakati
za mkoa na wananchi kwa ujumla.
"Bandari
ya Tanga, zao la mkonge pamoja na kukosekana kwa msukumo wa kuimarisha sekta ya
elimu ni moja ya masuala yanayoufanya mkoa huu kuzidi kurudi nyuma kiuchumi
pamoja na wananchi wake,” alisema Profesa Lipumba.
No comments:
Post a Comment