Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
WATU watatu, wakiwamo waandishi wawili, Hussein Semdoe wa gazeti la Mwananchi na Hamis Bwanga wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo na Ofisa Uhamiaji
wa Wilaya ya Handeni, Mariam Hassan wamefariki papo hapo katika ajali ya
kutisha iliyotokea leo Misima, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Marehemu Hussein Semdoe akiwa kazini. Picha hii ilipigwa mwishoni mwa wiki Kwamsisi wilayani Handeni mkoani Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu akiwa kwenye kazi za kijamii Kwedikabu, Kwamsisi mwishoni mwa mwaka jana. Mwenye Kamera ni marehemu Semdoe.
Watu hao walikuwa wakitoka Misima katika shughuli za kikazi
na kusababisha vifo hivyo vilivyopokelewa kwa uchungu mkubwa na Watanzania
wote, wakiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Afisa Elimu Shule za Sekondari
wilayani humo, Simon Mdaki, alisema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari
walilokuwa wanasafiria kupasuka tairi, hivyo dereva kulishindwa na kupinduka.
Alisema ajali hiyo ilikuwa nyuma ya gari ya Mkuu wa Wilaya
ya Handeni, Rweyemamu, aliyeambatana na watu hao ambao kwa sasa ni marehemu katika shughuli za
kikazi Misima.
Ni majonzi makubwa yaliyotokea leo baada ya kuwapoteza
Watanzania wenzetu, wakiwamo waandishi wawili na Afisa Uhamiaji ambao kwa
pamoja tunasikitishwa kutokana na vifo vyao vilivyotokea katika ajali hii ya
kutisha.
Mkuu wa Wilaya yeye hajaumia kwasababu gari lake lilikuwa la
mbele, ingawa ni msafara wake kwa pamoja, hivyo tumeguswa na vifo hivi
vilivyotokea katika wilaya yetu leo,” alisema.
Vifo vya waandishi hao ambao wana mchango mkubwa wilayani
humo vitakuwa ni pigo kwa Watanzania wote, wakiwamo wananchi wa Handeni ambao
kwa hakika mikono ya waandishi hao ilitumika vyema kuhabarisha umma kwenye
vyombo vyao.
Taarifa zaidi tutaendelea kuwapatia kadri tutakavyoendelea
kuzipata.
No comments:
Post a Comment