Na Mwandishi Wetu, Kilindi
WILAYA ya Kilindi mkoani Tanga, inatarajia
kupokea msaada wa chakula kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu jumla ya Tani 810, huku
tani 80 zikipangwa kutolewa bure kwa wananchi wasiojiweza, huku kingine kikisambazwa
kwa shule za Msingi na Sekondari na kinachobaki kuuzwa kwa Sh 50 kwa kilo kwa
familia zenye uwezo.
Mkuu wa Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa
Akizungumza jana mjini hapa,
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, alisema chakula hicho kinatarajiwa
kuanza kuingia kesho Aprili 14 kwa ajili ya kusambazwa kwa wananchi.
Alisema kufika kwa chakula
hicho ni sehemu ya serikali kupambana na njaa katika baadhi ya wilaya
zilizoathiriwa na njaa, ikiwamo Kilindi, ambapo viongozi wamekuwa wakifanya
juhudi kupambana nayo.
“Tunashukuru serikali kupitia
Ofisi ya Waziri Mkuu kutuletea chakula tanai 810 huku tukiona kuwa tutafanikiwa
kwa dhati kukabiriana na suala la njaa linaloziathiri kaya mbalimbali.
“Kwa wale ambao hawana uwezo
kabisa, tumewatengea tani 80, huku pia shule za msingi na sekondari zikipangwa
kuwa miongoni mwa watakaokuwa kwenye msaada huu,” alisema Liwowa.
Kilindi ni miongoni mwa wilaya
za Tanzania zilizokumbwa na suala la njaa, jambo linaloifanya serikali
kupambana nayo kwa kupeleka msaada wa chakula wilayani hapa.
No comments:
Post a Comment