https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, April 22, 2013

Angalia mikakati na picha mbalimbali za Miss Arusha City Centre


warembo wakali wa miss arusha city centre katika picha ya pamoja..
baadhi ya vimwana wa miss arusha city centre wakiwa kwenye mazoezi
mabebs wa ukweli kama vipi miss tanzania lazima atatokea hapa!!
opening show, !!
habari ya jijini arusha kwa sasa
Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji Kanda ya kaskazini, Miss Arusha City Center 2013, yanatarajiwa kufika kileleni usiku wa May 4 ndani ya hoteli ya Kitalii ya Snow Crest Hotel iliyopo jijini Arusha.

Akizungumza na Zeddylicious Blog, Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, amebainisha kuwa kila kitu kiko sawa na maandalizi yamekamilika, tayari kwa kumpata mshindi wa REDD'S MISS ARUSHA CITY CENTRE 2013

Muandaaji wa mashindano hayo alizidi kufafanua kuwa Warembo wote ni wenye mvuto na wenye vigezo stahiki na wako tayari kwa shughuli moja tu siku hiyo, anaongeza kuwa warembo hao wana ari kubwa ya ushindani, na kwamba kuna uwezekano mkubwa muwakilishi na mshindi wa Miss Tanzania 2013 akatokea kwenye kitongoji hicho.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...