https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, April 20, 2013

Eveline Kabwelile kupakua albamu ya Yesu Komando Mei 12



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
Msanii chipukizi wa Injili hapa nchini Eveline Kabwelile anategemea kuachia albamu yake ya kwanza aliyoibatiza jina la 'Yesu Komando' ikiwa na  jumla ya nyimbo tisa na kuirekodi katika Studio za Iki Production chini ya Producer wake Iki.
Mwimbaji chipukizi wa Injili, Eveline Kabwelile
Nyimbo hizo ni pamoja na  Yesu komando,   Ananitosha Bwana,  Mungu hawezi kukusahau,  Nakupenda Mokozi,  Mshukuru Mungu,  Ni wewe mwenyewe,  Usinipite Mokozi,  Mokozi asifiwe na  Ni Nani.

Albamu hiyo inategemewa kuzinduliwa Mei 12 mwaka 2013 katika Kanisa la Holiness Pentekoste kwa Mchungaji Ndalima Ubungo, kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na mbili jioni.

Akizungumzia sababu hasa iliyomfanya kuingia kwenye uimbaji wa Nyimbo za injili Eveline alisema kwa upande wake anasukumwa sana na wito wa Mungu kwani nilianza kupenda kuimba toka nikiwa mdogo na iko kwenye damu, yake

“Nilianza kuimba toka nikiwa mdogo sikumbuki ni mwaka gani, albamu hii nimeanza akuiandaa 2010  na 2011 ndio nikaanza kurekodi audio za nyimbo zangu na  nilianza kurekodi video za nyimbo zangu mwaka 2012 katika studio Brayanz work chini Byayan Hasani na nyimbo zote zimeshakamilika audio na video tayari kwa uzinduzi,” alisema.

Albamu ya audio na video ya albamu Yesu Komando itaanza kuuzwa siku ya uzinduzi.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...