Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimetangaza kuanza kwa
Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ya sita bora.
Msemaji wa DRFA, Mohamed Mharizo
Ofisa
Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, amesema hayo leo Aprili 5 kuwa ligi
hiyo itaanza Aprili 9 mwaka huu hadi 31 katika viwanja vitatu vya Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kinesi na Makurumla.
Alizitaja
timu zitakazochuana katika hatua hiyo kuwania kucheza Ligi ya Kanda
Taifa kuwa ni pamoja na Boom FC ya Ilala, Friends Rangers ya Magomeni,
Abajalo FC ya Sinza, Red Coast ya Mburahati, Day Break ya Magomeni na
Shariff Star ya Ilala.
“Kwa
mujibu wa ratiba yetu, kila siku kutakuwa na mechi tatu, hivyo katika
mechi za ufunguzi Aprili 9, Boom FC wao watachuana na Shariff Star,
kwenye Uwanja wa Airwing, wakati Day Break watamenyana na Friends
Rangers uwanja wa Makurumla huku Red Coast wao watacheza dhidi ya
Abajalo,” alisema Mharizo.
Wakati
huo huo, Mharizo amesema kabla ya kaunza kwa ligi hiyo, kutatolewa
semina elekezi kwa viongzi wa timu shiriki, itakayofanyika Jumapili
kwenye Ukumbi wa Shule ya BenjaminMkapa kuanzia saa nne asubuhi.
“Lengo
la semina hii elekezi ni kutoa elimu kwa viongozi na wachezaji ili
kuondoa mvutano wakati wa ligi hiyo, nia yetu ni nzuri na tunapenda
kuona ligi ikichezwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa,”
alisema Mharizo.
Semina hiyo itawahusisha Katibu, Mwenyekiti, Kocha, Nahodha na Waamuzi 16 watakaochezesha ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment