Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya Extra
Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern ndiyo burudani
zitakazonogesha tamasha la vyombo vya habari litakalofanyika Dar es
Salaam kesho Jumamosi, katika Viwanja vya Leaders Club badala ya TCC-Sigara Chang'ombe.
Akizungumza
Dar es Salaam jana, wakati wa kutambulisha burudani hizo, Mwenyekiti wa
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinachoandaa
bonanza hilo, Juma Pinto alisema maandalizi kuhusiana na tamasha hilo
linalojulikana kama Media Day Bonanza yamekamilika.
Alisema
wameichukua Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki na Jahazi Modern
inayoongozwa na Mzee Yusuph kutokana na makundi hayo kuwa juu hivi sasa
katika muziki kwa maeneo yao.
“Tunaamini
watakaokuja kwenye tamasha watakuwa na furaha ya aina yake na
tumejiandaa vya kutosha,” alisema Pinto na kueleza kuwa bonanza hilo
litafanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam na mgeni rasmi
atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Pia
Pinto alisema bendi ya Msondo Ngoma Music itapiga kwenye viwanja hivyo
kuanzia saa moja usiku baada ya bendi za Extra Bongo na Jahazi kumaliza
kutumbuiza Media Day na kwamba imetoa ofa kwa wanahabari watakaotaka
kubaki kuendelea kupata burudani mpaka usiku wa manane.
“Msondo wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na Msondo Ngoma,” alisema Pinto.
“Msondo wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na Msondo Ngoma,” alisema Pinto.
Bonanza
hilo la TASWA linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na
lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa
siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa
vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi
pamoja.
Kwa
upande wake Ofisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema wamejipanga vya
kutosha na kwamba wadau wafike kwa wingi kuhakikisha mambo yanaenda
kama yalivyopangwa.
“TBL
ni mdau mkubwa wa wanahabari, tumewaandalia mambo mazuri, naomba
msikose,” alisema Malulu na kuongeza kuwa wanaamini wadau 1,500 kutoka
vyombo mbalimbali vya habari wanaotarajiwa kushiriki bonanza hilo
watafurahi vya kutosha siku hiyo.
Naye
Choki akizungumza kwenye mkutano huo, alisema vijana wake wamejipanga
vya kutosha kushambulia na kuwa dhamira yao ni kuona wana habari
wanafurahi vya kutosha na kuwa mambo waliyowaandalia kila mtu atafurahi
kuiona Extra Bongo.
Taarifa za kubadilishwa eneo la kufanyika bonanza hilo zimejulikana leo na wadau wa TASWA, huku wajumbe wakitakiwa kueneza habari kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kuhamia kwenye viwanja hivyo vya serikali vya Leaders Club.
Taarifa za kubadilishwa eneo la kufanyika bonanza hilo zimejulikana leo na wadau wa TASWA, huku wajumbe wakitakiwa kueneza habari kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kuhamia kwenye viwanja hivyo vya serikali vya Leaders Club.
No comments:
Post a Comment