https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, April 18, 2013

Picha mbalimbali za msiba wa bilionea Babu Sambeke jijini Arusha jana

DSCF8828

Watu wakitoa heshima za mwisho
DSCF8830
Jaji Aisha nyerere msibani pamoja na mkurugenzi wa kibo palace Vicent Laswai
DSCF8832
Watu wakitafakari kwenye msiba huo uliogusa hisia za wengi jijini Arusha.
DSCF8848
Baadhi ya magari ya kifahari yaliyofika katika msiba huo
DSCF8847
Waombolezaji

Mamia ya vigogo pamoja na watu mbalimbali wafurika nyumbabi kwa marehemu Bilionea “Babu Sambeke”Ernest Sambeke eneo la njiro jijini Arusha kuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi huku msiba huo ukiwa tofauti na misiba mingine iliyozoekeaka hapa Nchini.

Marehemu,Sambeke alifariki hivi karibuni katika ajali ya ndege aliyokuwa akiiendesha na pia mmiliki wa ndege hiyo ambapo ilianguka katika eneo la Kisongo na kusababisha kifo chake Mkoani Arusha.

Shughuli za kuaga mwili wa marehu zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwaaajili ya mazishi.

Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka hapa Arusha na Moshi walionekana kutawala msiba huo.

Katika zoezi hilo la kuaga mwili wa mareheu Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu na baada ya kumaliza alitoa fursa kwa watu mbalimbali kupita mbele ya jeneza kwaajili ya kuaga mwili.
  Ndani ya jeneza marehemu alivalishwa nguo zake za kirubani huku, baadhi ya wanajeshi kutoka jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walionekana jana katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadhi yao walikuwa wamevalia sare za jeshi hilo.


Hatahivyo,baadhi ya watu walionekana katika hali ya kawaida huku watoto wakionekana na nyuso za huzuni mda wote.

Tofauti na misiba mingine nchini watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi vinywaji vya bavaria
Magari ya kifahari yalionekana kutawala msiba huo huku barabara ya njiro ikionekana kuwa na msongamano kubwa iliyosababishwa na zoezi hilo la uwagaji wa mwili
Marehemu aliacha watoto watatu ambao ni Sia,Jamal,Getruda.

 
Kwa hisani ya JAMII BLOG

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...