Ndugu Edward Moringe
Sokoine (01/08/1938-12/04/1984) alikuwa Waziri Mkuu wa aina yake nchini
Tanzania. Aliongoza katika kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu sana
ya kiuchumi. Leo ni miaka 29 toka Taifa limpoteze shujaa huyu. Katika kuenzi
fikra zake ambazo bado zinahitajika sana leo,
"Ole wake kiongozi
mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina
yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe
na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa
imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26
Machi 1983
"Juu ya suala hili la
mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa
wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo
hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23
Oktoba 1982
"Serikali inasimamia
bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei
ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei
yenyewe iweze kujirekebisha" - Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba
1983
"Wajibu wa kila
Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa
Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama
hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada
kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983
"Vijana leo wengi wana
mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini
wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi
asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23
Oktoba 1983
"Katika nchi inayojali
haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya
walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali
nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari
1977
No comments:
Post a Comment