LADHA KUTOKA KWA WASANII WETU
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HII ni siku nzuri kwangu, huku nikiamini pia kwa upande wako
itakuwa tamu kupita kiasi kutokana na kudra za Muumba wetu. Katika hilo,
naamini utaendelea kuwa na mimi katika kona hii ambayo ilikuwa ikitoka katika
blog hii ingawa ilisimama kwa muda.
Mwimbaji wa Baba Awena, Vida
Kuna mengi ambayo tunatarajia kuyafanya lakini tunajaribu
kuweka kwanza mipango kwa namna moja ama nyingine. Kwa kulijua hilo, kona ya
LADHA KUTOKA KWA WASANII WETU ni kati ya zile ambazo nahitaji ziendelee kuwapo
kwa ajili ya kupata ladha za mashairi ya wasanii pamoja na kujua maana japo kwa
uchache tu.
Kona hii itakuwa inatoka mara moha kwa wiki ili kupisha
utaratibu na mpangilio mwingine uendelee katka blog hii ya Handeni Kwetu. Ndugu
yangu, katika jamii wapo watu ambao wanalia na kusaga meno katika suala zima la
mapenzi.
Kwa bahati mbaya, wengi hatuna uwezo wa kutembea mbele za
watu na kutangaza jinsi tunavyoumizwa kwenye uhusiano wetu. Pamoja na hayo,
wapo wasanii ambao huvaa uhusika na kutuwakilisha mbele ya hadhira kwa kuimba
au kuigiza kinachofanana na sisi.
Katika wimbo wa Baba Awena ambao umeimbwa na Vida anayetokea
katika
Taasisi ya Kukuza Vipaji Tanzania House of Talent (THT) akishirikiana na
Linex, wameonyesha jinsi gani wawili hao wanavyolilia uhusiano wao usipotee.
Msichana anasema madhira yanamtesa na chanzo ni mapenzi.
Hana amani wala furaha katika moyo wake kiasi cha kujiuliza kama kupenda ni
makosa. Na kama kweli ni makosa basi aambiwe kuliko kuendelea kuumia moyoni
mwake.
Mwanadada anasema kujiachia kwake kwa kuonyesha mapenzi kwa
mtu wake kumeleta dharau kiasi cha kuonekana mtaani kama yeye ni muhuni.
Anahitaji sasa kufahamu kila kinachoendelea katika uhusiano huo.
Nyimbo inaimbwa kwa kupokezena na Linex, huku jamaa huyo
akijaribu kumlainisha mpenzi wake kwa kumueleza kuwa mbona yeye naye yupo
moyoni mwake. Anasema anahitaji nafasi ya kuonyesha mapenzi ya ukweli.
Anaongea mengi, lakini mwanadada anasema kama kweli mshikaji
ni chanda chema, iko wapi thamani yake? Ina maana bado hajajua ni vipi penzi
lake linakwenda. Anajionea mawenge tu. Hii ni hatari aisee katika suala la
malavidavi.
Katika kuliangalia hilo, ni vyema sisi wadau au jamii kujua
kuwa tunapokuwa kama sigara kali, hatueleweki, kwenye mapenzi tunatesa watu
wenzetu. Tuwaonee huruma basi. Tuwe makini nao jamani. Nao wana moyo kama yetu.
Wanaumia.
Kwanini? Kuna mijamaa mingine ikishaona inapendwa weee acha
tu. Wanatembea mabega juu. Wakipigiwa simu na mademu zao wanabinua midomo kama
vile wao ndio mashori. Kwanini? Acheni kudengua jamani.
Kabla ya kuzama zaidi mwisho wadau waone huyu msela
anachooonga, basi tuanze kuyapitia haya mashairi ya Vida na Linex kama
yanavyokujia.
Mama mama awena, wena, awenaaaa
Kutenda kosa, sio kosa
Kurudia kosa ndio kosa
Kuruhusu mutima wawnyuma, kunjutia kubony kunamaaa
Ubeti 1
Ungelijua madhira, yanavyokera moyoni
Kitaa kizima naonekana kama vile m muhuni
Ungelijua madhira, yanavyokera moyoni
Kitaa kizima naonekana kama vile m muhuni
Lisilofaa kutendwa usimtende mwenzako
Ohooo naumia mpaka kumoyo
Ohooo naumia mpaka kumoyo
Kiitikio
Kufumba kufumbua ooo baba awena
Tayari jiji ushalijua ooo baba awena
Ohooo baba awena, ohoo baba awena
Ooo baba awena, ooo baba awena
Ubeti 2
Linex+Vida
Naihitaji nafasi nyingine yakujishusha ngazi
Ibakila vyoose venda koseeee
Nilikubali niwe wako nikakupa mutima gwangu wee
Kama kweli wee chanda change iko wapi thamani yangu
Kama kupenda ni makosa, niambie ukweli nijuwe
Hapa mjini kutafuta, kesho lukwili unitimuwe
Ooooo naumia mpaka kumoyo
Ohooo naumia mpaka kumoyo
Kiitikio
Kufumba kufumbua ooo
baba awena
Tayari jiji ushalijua ooo baba awena
Ohooo baba awena, ohoo baba awena
Ooo baba awena, ooo baba awena
Baba awena, baba awena baba wee nihurumie
Baba awena, baba awena baba wee nihurumie
Haitakuwa rahisi kukufuta akilini ehee
Maneno unayosema yananifanya nitamani
Ardhi ipasuke niingie eheeee (Nijifiche)
Kama kupenda ni makosa, niambie ukweli nijuwe
Hapa mjini kutafuta, kesho lukwili unitimuwe
Kitikio
Kufumba kufumbua ooo baba awena
Tayari jiji ushalijua ooo baba awena
Ohooo baba awena, ohoo baba awena
Ooo baba awena, ooo baba awena
No comments:
Post a Comment