https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, April 18, 2013

AUNT EZEKIEL: JAMANI NIMECHOKA KUTONGOZWA OVYO NA BAADHI YA WABUNGE

MKALI wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel ameinua kinywa chake na kudai kwamba kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kupata penzi lake, hivyo kumsumbua katika ndoa yake.
 
Akizungumza juzi jijini Dar, Aunt alisema waheshimiwa hao wanajua tayari yeye ameshaolewa lakini wamekuwa wakimpa usumbufu mkubwa na kutoa ahadi balimbali, ndogo na kubwa kitendo ambacho anaamini kinaweza kuhatarisha ndoa yake.

“Mimi nawashangaa sana baadhi ya waheshimiwa, wanajua tayari nimeolewa lakini wananitongoza, mimi siwezi,” alisema Aunt bila kuwataja majina wazito hao Akaongeza: 
 
“Mume wangu akisikia napata usumbufu kutoka kwa watu wazito, hawezi kuwa na amani, bado naipenda ndoa yangu na kuachana na Sunday wangu ni ndoto.”

Mwishoni mwa mwaka jana, Aunt alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunday Dimonte, Dubai na mpaka sasa wanaishi kama mke na mume wake. Stori hii ni kwa hisani ya LENZI YA MICHEZO BLOG.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...