Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI kongwe na pendwa ya muziki wa dansi nchini Tanzania, The
African Stars ‘ Twanga Pepeta
Internatinal’ inatarajiwa kuporomosha bonge la shoo ndani ya Jiji la
Mwanza katika tamasha la la kihistoria la utamaduni wa Msukuma
lililopangwa kufanyika Mei 27.
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka
Akizungumza jana Mtaribu wa tamasha hilo ambayepia ni Naibu Mkurugenzi wa
Kampuni ya May Way Entertainment Rose Mwita alisema bendi iyo itafanya
maonesho mawili ambapo baada ya CCM Kirumba siku itakayofuata Mei 28 watakuwa
katika mji wa Nansio Ukerewe
katika tamasha la kihistoria la utamaduni wa mkerewe matamasha yote
yatafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka usiku.
Mwita alisema bendi ya Twanga Pepeta imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii
na maendeleo ya vijana kupitia muziki. Hivyo, burudani ya bendi hii na burudani
nyinginezo zitakazokuwepo ili kuhamasisha wakazi wa Mwanza na Ukerewe
kuhudhuria kwa wingi.
Rose alisema, “Tamasha hili
linalenga kuhamasisha jamii ya msukum na mkerewe na makabila mengine
kuenzi mila na tamaduni. Vilevile, jamii na familia zilizopo ndani na nje ya
mikoa yao zikumbuke nyumbani na kutembelea wazee mara kwa mara pamoja na kuezi
mila na utamaduni wa kwao”.
Aliongeza kwa kusema kuwa, zaidi ya watu 3,000 na familia zao, wanatarajiwa
kuhudhuria kwa wingi katika matamasha hayo yenye mvuto wa kihistoria huku
wakipata fursa ya kusikia historia ya msukuma na mkerewe kwa kina toka kwa
wazee wanaotoka sehemu mbalimbali hasa kwenye familia za watemi wa Kisukuma na
Wakerewe.
Maonesho mengine yatakayokuwepo ni pamoja na kuona maonyesho ya zana za
kale za jadi zilizotumiwa na makabila haya mawili, kucheza ngoma zote za
asili ya msukuma na mkerewe pamoja na vikundi tofauti tofauti vya ngoma za
asili na sanaa za makabila mengine vyakula vya aina zote na vya asili ya
msukuma na mkerewe. Vinywaji vyote vya asili ya msukuma na mkerewe.
Mwita alisema pia katika kunogesha tamasha hilo kutakua na burudani
toka kwa wasanii wa kizazi kipya kutoka Dar es Salaam.
Vilevile alisema, wamewaalika viongozi wa serikali yetu, viongozi wa dini
zote, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya mkoa wa Mwanza,
viongozi wa asasi zisizo za kiserikali za serikali na wanafunzi kutoka vyuo na
shule mbalimbali katika mkoa wa Mwanza.
Wadhamini wa tamasha hili ni pamoja na
Balimi Extra Lager, Safari Lager, Pepsi, Star TV, Redio Free Africa, JB Belmont
Hotel, Mwanza Institute, Toyo na La Kairo Investiment.
No comments:
Post a Comment