Na Mwandishi Wetu, Morogoro
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatarajiwa 'kuuteka' mji wa Gairo kitakapofanya
mkutano mkubwa wa hadhara kuanzia saa kumi jioni katika mji huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Kulingana
na shamrashamra na simulizi zilizvyotanda miongoni mwa wananchi katika maeneo
mbalimbali hapa Gairo, mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu,
kwa ajili ya kumshudia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye anakuwa
Gairo kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kushika wadhafa huo.
Mbali
na Kinana ambaye aliwasili jana jioni, akitokea Kilosa, viongozi wengine
wanaotarajiwa kuwasha moto kwenye mkutano huo,ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Dk.
Mohammed Seif Khatib.
Kabla
ya mkutano huo Kinana na ujumbe wake wamepangiwa kufanya shughuli mbalimbali
za ujenzi wa Chama na ukaguzi wa ilani ya CCM, ikiwa ni pamoja na Kinana
kufanya kikao cha ndani na mabalozi na viongozi wa Chama ngazi wa kata
zioizopo karibu na makao makuu ya wiyala.
Kaim
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda amesema asubuhi hii kiwamba,
baada ya mkutano wa ndani, Kinana atafanya shughuli ya kukagua uhai wa chama
katika mashina na matawi katika maeneo mbalimbali wilayani hapa.
|
No comments:
Post a Comment