Mwili wa dereva wa lori
moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari
kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina
moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani ya gari hilo wakati vijana wengine
wakiendelea kupakia moram asubuhi ya leo
Baadhi ya wananchi
waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na
wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo halikupata
nafasi
Meya wa Manispaa ya
Arusha, Mh Gaudence Lyimo akisaidiana na vikozi vya jeshi katika zoezi la
uokozi
Mh Lema akiangalia
namna vikosi vya Jeshi la Wananchi pamoja na askari Polisi wakiendelea na zoezi
la uokozi
Mwananchi huyu
aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka
kwenye kifusi
Hali ilivyo
machimboni hapo
Kina mama wakilia kwa
uchungu wakihofu kuondokewa na wapendwa wao
Vikosi vya Jeshi la
Wananchi na Polisi vikiwa kazini
Sehemu ndogo ya Fuso
ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa
Ambulance ya Jiji
tayari tayari kwa lolote ikihitajika
Wachina wakielekea
eneo la jali na vifaa vyao kusaidia zaidi zoezi la
uokozi
Wanajeshi zaidi
wakielekea chini kwenye mgodi
Tunaomba radhi kwa ubora
hafifu wa picha hizi….
KWA mujibu wa mashuhuda
wa ajali iliyotokea leo asubuhi Jijini Arusha, inakadiriwa zaidi ya watu 18
wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba
na kupakia kwenye malori.
Ajali hiyo mbaya
imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya Jiji eneo jirani na
Moshono-Kiserian ambapo vijana hao wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa
wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani
18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na kifusi. Shuhuda mmoja wa ajali
ambae pia ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama
Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva na
utingo.
Blog hii iliweza
kushuhudia sehemu ndogo sana ya Fuso ikionekana lakini gari nyingine ilikua
imefukiwa kabisa na kupondeka vibaya. Miongoni wa waliofikwa na
mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. taarifa za eneo la tukio zinaeleza
utingo mmoja ameokolewa akiwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali lakini
dereva wake amefariki dunia.
Katika eneo la ajali
hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki
na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa Manispaa Mh
Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni miongoni mwa
viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la
Wananchi kufanya uokozi.
Blogu hii ilishuhudia
pia Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika
kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi
hicho.
No comments:
Post a Comment