https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, April 10, 2013

Zitto Kabwe amlima barua nzito Spika wa Bunge, Anne Makinda


"Nimeandika barua Kwa Spika wa Bunge kutaka Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo Bungeni kuhusu uamuzi wake wa kuwapa leseni kubwa ya kuchimba #Uranium huko wilayani Namtumbo. 
Zitto Kabwe
Mnamo tarehe 10 Agosti 2013 Waziri alitamka ndani ya Bunge "sisi tunajua zaidi ya anavyojua yeye, Leseni haijatolewa na haitatolewa mpaka Kampuni ya MantraResources ilipe kodi".


Kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) ya $189m kufuatia mauzo ya mradi wa Mkuju RiverProject kutoka kampuni ya Mantra kwenda kampuni ya AMRZ ya Urusi iligomewa kulipwa. 

TRA wamepeleka shauri hilo mahakama ya kodi na mpaka sasa maamuzi hayajatolewa. Kwa mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2012, kabla ya Waziri mwenye dhamana ya madini kubariki mauzo ya kampuni, anapaswa kupata Kibali Cha kwamba kodi zote stahili zimelipwa. 

Kibali Kwa kampuni ya mantra kilitolewa bila kujali hitaji la kisheria na sasa kampuni hii imepewa leseni.


 
Maamuzi haya ya Waziri wa Nishati na Madini yanalikosesha Taifa mapato ya zaidi ya tshs 300bn ambazo zingeweza kumaliza tatizo la nyumba za walimu nchi nzima na kulipia madai yote ya walimu. 

Fedha hizi zingeweza kujenga barabara ya lami kutoka Manyoni mpaka Itigi. Fedha zingeweza kukarabati reli ya Kati na kuirejesha katika ubora wa unaotakiwa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge nimetaka Waziri atoe maelezo bungeni na wabunge wajadili. 

Ni dhahiri kwamba serikali inayoongozwa na CCM imeamua kumaliza utajiri wote wa nchi na kuugawa Kwa wageni Kwa bei ya Che. Wananchi Ni lazima kusimama imara kukataa uporaji huu na maamuzi haya ya kiburi Cha kudharau Bunge yaliyoyafanywa na Serikali."

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...