Nyosh El Sadaat, kiongozi wa Wazee wa Ngwasuma
BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, Alhamisi hii inatarajia kufanya
onyesho la nguvu katika Ukumbi wa Aventure, uliopo mjini Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Kufanyika kwa shoo hiyo katika mji wa Moshi ni mipango ya
bendi hiyo kuwapatia burudani mashabiki wao, ukizingatia kuwa muda mrefu
wanaishi Dar es Salaam,
hivyo kuwabagua wadau wao wengine.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba mashabiki wao wa Moshi wajiandae
kupata vitu adimu kutoka kwa vijana wake wenye uwezo wa hali ya juu.
Alisema kwamba wanamuziki wao wamejipanga kuhakikisha kuwa
mashabiki wao wanapata kitu adimu kutoka kwao, hivyo waende kwa wingi kuangalia
kazi nzuri za vijana wao.
“Tunafanya shoo ya nguvu katika ukumbi huo ambao naamini
tutawaacha watu katika shangwe za aina yake, ukizingatia kuwa tuna vyimbo nzuri
na utundu wa kuimba kwa kiwango cha juu na jinsi ya kuwapa raha mashabiki wetu.
“Waje kwa wingi kujionea jinsi Wazee wa Ngwasuma
wanavyofanya mapinduzi katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, bila
kuangalia ushindani uliopo na wale tunaoshindana nao kila siku ya Mungu,”
alisema Mkinga.
Bendi hiyo ipo chini ya Rais wa Vijana, Nyosh El Saadat,
akiwa na waimbaji wengine mahiri, akiwamo Patchou Mwamba anayewika pia katika
tasnia ya filamu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment