Friday, December 07, 2012
Unalijua Hombo?
UTAMADUNI
TANZANIA yenye zaidi ya makabila 120, kila moja lina utamaduni wake. Kutokana na hilo, unaweza kumuona mtu katika hali fulani, lakini utamaduni wake, au mazoea yake yakakushangaza na kumuangalia mara mbili mbili.
Kama alivyokutwa na MpigaPicha wa Handeni Kwetu leo mkazi wa Sinza, Jijini Dar es Salaam, Rehema Mbwana, alivyokutwa akionja mboga aina ya hombo, katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Kijiji hiki kinakaliwa na makabila mchanganyiko, lakini wenyewe haswa ni Wazigua wanaounda kwa pamoja wilaya ya Handeni ambayo kwa sasa Mkuu wake wa Wilaya ni Muhingo Rweyemamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment