Na Fadhili Athumani, Moshi
07, Desemba
MSANII anayefanya vizuri katika Tasnia ya Bongo Movie,
Patcho Mwamba, amesema uvumi unaoenezwa kwamba ameanza kupoteza muelekeo katika
tasnia hiyo kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu ni kelele za chura ambazo
yeye binafsi hazimzui kunywa maji na kusisitiza Patcho atabaki kuwa Patcho.
“Kuna watu wanasema kuwa Patcho alikuwa anabebwa na the
Great, wengine wanasema Patcho ameishiwa, watashangaa tena watashangaa sana,
kuna kazi za watu nazimalizia na mara baada ya hapo natarajia kutoa saprize kwa
mashabiki ya Patcho,” alisema Patcho
Akizumzungumzia Marehemu Steven Kanumba, Patcho alisema katika
Tasnia hii ya Bongo Movie hakuna mtu wa kufafananishwa na Marehemu na
kusisitiza kwamba hata angeambiwa atunge mashairi ya kumsifia Kanumba kwa jinsi
anavyomfahamu, asingeweza kumaliza sifa za Kanumba.
“The Great atabaki tu kuwa the great, kwa Afrika sioni mtu
kama yeye na hakuna mtu ya kufanana na Kanumba, kuna mengi sana ya kuzungumza kuhusu
swaiba lakini hata nikiambiwa nitunge mashairi siwezi maliza sifa zake, Kanumba
acha tu,” alisema Patcho
Patcho Mwamba kwa kuonesha mapenzi yake na heshima yake kwa Kanumba,
bado hakusita kumwagia msanii huyo nguli wa Bongo Movie aliyefariki Aprili 14
mwaka huu, na alipopanda jukwani Patcho aliwaliza washabiki pale alipokuwa
akiimba wimbo mpya wa bendi hiyo wa Maisha na kusema hakuna rafiki wa kudumu
hapa duniani wala adui wa kudumu huku akimtaja Kanumba kila mara.
Patcho alisema ukimya wake unamaana kubwa na hivi karibuni
wale wote wanao eneza uvumi huo watashangaa kwani kwa sasa kuna kazi za watu
aliyoshirikishwa anazozimalizia na mara baada ya hapo pamoja na kubanwa na kazi
za kutangaza staili mpya bendi yake kuna filamu ziko jikoni ambazo anategemea
kuzingiza sokoni mapema mwakani.
Mbali na sanaa ya uigizaji Patcho Mwamba, aliyeibuliwa na
Marehemu Kanumba, pia ni mwanamuziki na muimbaji wa kutumainiwa katika bendi ya
FM academia “wazee wa Ngwasuma” na baadhi ya kazi alizowahi kufanya katika
tasnia ya filamu ni pamoja na Uncle JJ, Young Billionaire, Devils Kingdom na
nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment