Yameandikwa na Rashid Hassan Kilo, kutoka kijiji cha Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga katika mtandao wa facebook.
HAYA ni malalamiko ya watu wa kijiji cha Misima, wilayani Handeni mkoani
Tanga, yameandikwa na Rashid Hassan Kilo, nikaona niyapachike hapa
kutoka kwenye wall yake...... Sijaongeza wala kupunguza...
Habari za asubuhi "Wana wa Handeni"
Kwangu kumekucha salama hofu na mashaka ni kwenu. Hoja yangu leo ni juu
ya matangazo yaliyozagaa kila kona ndani ya mipaka ya kijiji cha Misima
yanayohusu kuchangia ujenzi wa maabala ya shule ya sekondari Misima
katika mchanganuo ufuatao:
1. Nguvu kazi 10,000@
2. Ng'ombe 3000@
3. Mbuzi/kondoo 1000@
Labda niishie hapo kwanza kwakuwa mlolongo ni mrefu sana kwani ni zaidi
ya vipau mbele 26 na viwango tofauti vya kulipia. Mwisho ni jina
Mtendaji wa kijiji
S. KIDUNDA
VEO-MISIMA.
Japo tunajuwa haya
ni maendeleo lakini kwanini tusingeitishwa mkutano na kupata ufafanuzi
juu ya ghalama za ujenzi wa maabala hiyo, gawanya kwa idadi ya watu,
mifugo, maduka, migahawa na vyanzo vyote vya vijiji 5 vya kata ya
Misima?
Katika ibara ya 18(d) ya Katiba tuanayotumia sasa ya
1977 "Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu
masuala muhimu kwa jamii."
Leo hili lakujenga maabala ni tukio
muhimu sana kwetu na kwa vizazi vyetu ila jinsi ya uongozi wa kiimla wa
Misima unavyotufanyia umeyatokomeza na unazidi kuyatokomeza kabisa
maendeleo ya Misima.
Leo hii ni miaka mingi imepita bila
kusomewa mapato na matumizi, lakini pia ni zaidi ya mwaka 1.6 tangu
18/10/2012 hatujafanya mkutano kwa viongozi kutuogopa kwa maovu yao, leo
hatupo tayari kuchangia bila kupata mchanganuo unaoeleweka lakini pia
hatupo tayari kutoa pesa kwa kwa viongozi wasio waaminifu.
Lakini la mwisho kiwango kilichowekwa ni kikubwa bora ingekuwa kila kaya
10000, lakini nguvu kazi? Kwa kipindi hiki ambacho wachangiaji wenyewe
wanategemea chakula cha msaada toka serikalini? Ningeomba viongozi
wangefanya mkutano kwanza na wanakijiji ili kujadiliana kwanza kuliko
kutuogopa, mtatuogopa hadi lini?
No comments:
Post a Comment