Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa zamani wa timu ya Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’,
amesema kwamba mara kadhaa makocha wa Tanzania wanafanywa kama makatapila
katika klabu kubwa, zikiwamo Simba na Yanga.
Kocha Jamhuri Kihwelo Julio
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati anapewa cheti
cha kushiriki kozi ya makocha iliyofanyika mjini Zanzibar, Julio alisema hali
hiyo hutokea na kutokana na kuhitajika katika timu kabla ya kutimuliwa
atakapopatikana kocha mwingine.
Alisema ingawa makocha wanakutana na changamoto hizo, lakini
wao wamejipanga kuhakikisha kuwa wanakabiliana na matatizo yote katika timu
hizo kwa ajili ya nafasi zao kuwanufaisha Watanzania wote.
“Mimi siangalii matatizo hayo, ingawa tunajua kuwa tunaitwa
katika timu zetu kuwachongea barabara
wengine wanaokuja kurithi mikoba yetu katika timu nyingi.
"Sisi hatuna tofauti na makatapila, lakini hatuna wasiwasi
katika hilo, maana kwa upande wangu nimekuwa na ndoto na uwezo wangu
kuwanufaisha Watanzania, ndio maana najiendeleza kila mara,” alisema Julio.
Aidha, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),
Selestine Mwesigwa, aliwataka makocha wa Tanzania kuwa na moyo wa kujiendeleza
ili wajiweke katika mazingira mazuri zaidi katika majukumu yao ya kila siku.
“Kwa makocha wa Tanzania wao ndio huimudu lugha mama ya
Kiswahili, hivyo wanapojiendeleza kidogo kwa kuchukua kozi mbalimbali wanakuwa
kwenye soko kubwa na huwa nafasi ya kukuza mpira wa miguu hapa nchini,” alisem
Mwesigwa.
No comments:
Post a Comment