MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Simba SC, leo wanashuka
katika Dimba la Uwanja wa Taifa kuvaana na Wakata miwa wa Mtibwa Sugar, yenye
maskani yao Turiani mkoani Morogoro.
Picha hii ikiwaonyesha wachezaji wa Simba, wakijinoa.
Mchezo huo wa kirafiki unaosubiriwa kwa hamu na mashabikiwa
kandanda, unafanyika kama sehemu ya kuviandaa vikosi hivyo vimavyojiandaa pia
na patashika ya Ligi ya Tanzania Bara, ambapo hatua ya mzunguuko wa pili
inaanza Januari 25 mwaka huu.
Mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni, unafanyika huku Simba
wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kushindwa kutwaa taji la Kombe Mapinduzi lilomalizika
hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, huku makocha wa pande
zote mbili wakitambiana kuwa wote wataonyesha soka safi na lenye kusisimua
mashabiki wa kandanda Tanzania.
Kocha wa Simba, Zdravko Lagarusic, alitamba kuwa kikosi
chake kitaonyesha soka safi kwa ajili kuwapatia burudani mashabiki wao.
“Kikosi changu kipo vizuri na mazoezi tuliyofanya wiki nzima
yamenipa jeuri ya kupata ushindi dhidi ya wapinzani wetu hao,”alisema
Naye Mack Mexime aliwahakikishia wadau wa Mtibwa Sugar kuwa
ushindi mbele ya Simba ni lazima, ingawa wanacheza mechi ya kirafiki.
No comments:
Post a Comment