Na Kambi Mbwana, Dares Salaam
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhan Madabida leo atakuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Diwani
Cup yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mbagala Kuu, iliyopo
katika Kata ya Mbagala Kuu.
Timu za Kuzazi na Sansiro kutoka kata hiyo zitapambana
kuwania zawadi ya kombe, ng'ombe na jezi seti ambazo ni zawadi za mshindi wa
kwnza.
Madabida ndiye atakayekabidhi zawadi ya mshindi wa kwanza na
ile ya pili ambaye ataondoka na jezi seti moja huku msindi wa tatu atapewa jezi
seti moja.
Akizungumza jana, Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu,
Benson Malawandu, ambaye ndiye mwandaaji wa mashindano hayo alisema fainali
hiyo inatarajiwa kuwa ya aina yake kutokana na kukutanisha timu zenye upinzani
wa jadi.
Alisema kilichopelekea kumwalika Madabida katika mashindano
ni kutokana na kiongozi kuwa ni mpenda michezo ambaye amekuwa akitoa
kuhakikisha anasaidia vijana.
Malawandu akizungumzia mashindano hayo kwa ujumla alisema kwa
kiasi kikubwa malengo yametimia.
Alisema wakati anayaanzisha alikuwa na malengo ya kukutanisha
vijana pamoja, kutoa fursa kwa vijana kutumia michezo kwa ajili ya kujenga
mshikamano na kuepukana na kukaa kwenye magenge.
"Malengo ya mashindano haya kwa asilimia kubwa
yamefanikiwa sana, na ndio maana hata zawadi za washindi zilianza kutoka katika
hatua za makundi kila timu iliiyoongoza ilipata jezi seti moja na mpira na zile
za pili zilipata mipira," alisema.
"Pia kila timu iliyoshiriki nilitoa mpira mmoja kwa
ajili yao kujiandaa, na katika hatua ya robo fainali kila timu pia ilipata
zawadi ili kuongeza morali ya mashindano, aliongeza.
Pia alisema lengo lingine lilikuwa ni kukamilisha ilani ya
chama chao ambacho kinaichukulia michezo kama ni ajira tosha kwa vijana ambayo
inaweza kuwakomboa kiuchumi.
Wakati huo huo Malawandu alisema mashindano hao kuanzia sasa
yatakuwa ni endelevu na ana mpango wa kuyafanya kila mwaka huku pia kwa sasa
akijipanga na kamati yake kwa ajili ya kuanzisha na wanawake.
No comments:
Post a Comment