https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, January 25, 2014

Matukio katika picha ya mazishi ya Mbunge wa Chalinze Bwanamdogo

 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Miono leo wakati wa shughuli za maziko.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiweka udongo kaburini.
 Askari wa Bunge wakibeba jeneza kuelekea kaburini wakati wa maziko.
 Viongozi wakijumuika na waombolezaji makaburini.
 Waombolezaji wakishiriki kuomba dua nyumbani kwa marehemu.
 Baadhi ya waombolezaji wakishiriki shughuli hiyo nyumbani kwa marehemu.
Dua.....
Rais Kikwete akiagana na waombolezaji baada ya kutoka msikitini.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...